Wednesday, January 14, 2015

Kuongea na Wasiofikiwa



KANUNI ZA KUONGEA NA WATU WALIO TOFAUTI NA UTAMADUNI WAKO
I.             KANUNI: Kanuni kubwa ya ushuhudiaji au uinjilisti unapoongea na mtu mwenye imani au utamaduni tofauti na wako ni: ANZA NA ANACHOJUA NA MALIZIA NA ASICHOJUA (AMBACHO WEWE UNAKIJUA).

 Kwa mfano
1.   Ukiongea na Mmeru au Mchaga ambaye hajaokoka anza na kuelezea masale na kazi yake ya upatanishi, kabla hujaongea kuhusu damu ya Yesu na upatanishi. Tafuta kitu fulani katika utamaduni wake ambacho kitakusaidia kuelezea wokovu.

2.   Ukiongea na Mmasai anza na mfano wa mungu mweupe na Mungu mweusi, kisha mweleze Mungu ni mmoja naye amejaa nuru, mwambie Mungu anayesema ni mweupe wa kweli ni Mungu aliyemtoa Yesu msalabani ili roho za watu ziwe nyeupe. Usimseme vibaya mungu wake, bali mseme vizuri Mungu wa kweli unamtaja mungu wake kwa kutafuta mlango au daraja la mawasiliano katika utamaduni wake.
Paulo alitumia kanuni hii alipokuwa Athene alianza na kitu walichojua wao. Katika madhabau yao waliandika “kwa Mungu asiyejulikana” (Matendo 17:23). Yeye akasema ameona imeandikwa hivyo, hilo walikuwa wanalijua Waathene, halafu akaanza kuwaelezea wasilo lijua yaani Mungu wa kweli. Alitumia jambo wanalolijua kama daraja, au mahali pa kusimamia kusema. Petro pia alipoongea na Wayahudi (Matendo 2) aliongea nao kwa kutumia Torati, Torati ilikuwa ndicho kitu wanachojua, kisha akamsema Yesu.

II.           KANUNI: Katika utamaduni wowote kuna ishara za kiungu ndani yake ambazo zinaweza kutumika kama madaraja ya kusema ukombozi wa Yesu. Pia uumbaji wa Mungu unaoonekana unaweza kutumika kama kitu wanachojua kuwaeleza wasichokijua. Paulo na Barnaba (Matendo 14: 8-18), walimwombea kiwete huko Listra akatembea. Watu wa pale wakatafsiri tukio hilo kuwa ni miungu yao (herme na  zeu), kuwa ndiyo imefanya muujiza. Paulo wakamwita herme na Barnaba zeu. Walifanikiwa kuwatoa kaitka Imani hiyo kwa kutumia mazingira wanayojua ya mvua na chakula hata wakaweza kuwasiliana nao. Maandiko yanasema, “Lakini Mungu hakujiacha pasipo ushuhuda, kwa kuwa alitenda mema, akiwapeni mvua kutoka mbinguni na nyakati za mavuno, akiwashibisha mioyo yenu chakula na furaha” (Matendo 14:17).

Kaitka kila utamaduni wa wasioamini kuna ushuhuda wa kimungu, uwezao kutumika kushuhudia.
1.   Uumbaji wa Mungu wanaoujua
2.   Utamaduni wao hasa nini wanaamini
Kabla ya kuongea na asiyemjua Yesu au kusikia Injili
1.   Tafuta kujua anaamini nini
·         Tafuta vitu gani katika imani yake vianafanana na ukombozi wa Yesu
·         Katika hivyo mseme Yesu
2.   Tafuta kujua anategemea kitu gani sana katika uumbaji je ni maji? Asali? Nk katika hayo tumia kumhubiri Kristo
3.   Shiriki naye utamaduni wake ambao si kinyume na maandiko, mfano kula alacho hata kama ni nyoka ili umpate, Paulo alikuwa hali zote kwa wote ili awapate (1Wakorintho 9:22-23)
4.   Jifunze lugha yao, maana lugha ni sehemu kubwa ya utamaduni
5.   Tegemea nguvu za Roho Mtakatifu miujiza itokee, miujiza ni daraja kuwa la mawasiliano kwa wasioamini.

No comments:

Post a Comment