Sunday, January 4, 2015

Ufahamu katika Maombi

WAKATI NINAOMBA NILIFAHAMU MAMBO YAFUATAYO:

1.Yesu aliharibu mamlaka ya Shetani juu ya watu, akawa na mamlaka yeye juu ya watu. Kwa haya aliyofanya ndio maana akasema anazo funguo za mauti na za kuzimu (Ufunuo 1:18).

2.Kwa kufa kwake aliharibu mamlaka ya Shetani, kwa kuwa hai kwake akawa na mamlaka juu ya wanadamu(Yohana 17:2).

3.Maandiko yanaonyesha Mungu kwa njia ya Yesu ametukomboa toka mamlaka ya giza, amefanya hivyo kwasababu anazo funguo, Shetani na mamlaka yake hakuweza kuzuia.

4.Adam wa mwisho ni Roho mwenye kuhuisha, Anaondoa mauti. Palipo na giza anahuisha na kuleta nuru. Palipo na dhambi anahuisha na kuleta utakatifu. Palipo na uongo anahuisha na kuleta kweli (1Wakorintho 15:45).

5. Mwili wa Adam uliolala kama mavumbi, Mungu alipoupulizia pumzi ya uhai ilikuwa ni mfano wa roho ya Kristo. Mifupa ya Ezekiel 37, ni mfano wa roho ya Kristo. Roho ya Yesu inavifanya vitu viwe hai. Yesu ni Pumzi inayofanya vitu viwe hai. Mungu aliposema nchi na ijawe na viumbe hai (Mwanzo 1:24), bila shaka ilikuwa ni Roho ya Kristo iliyotenda.

6.Yesu alipotoka katika mwili na kwenda kuzimu kuharibu  mauti, aliporudi duniani, mwili wake ukahuishwa ukawa mpya. Kifo kililetwa na Adamu, ndio maana alikufa. Ufufuo umeletwa na Yesu, ndio maana amefufuka. Alikufa afanane na Adamu akafufuka tufanane naye(1 Wakorintho 15:35-49).

7. Chochote cha Shetani Yesu alichokifunga alipokufa, hakuna awezaye kukifungua. Chochote alichofungua ndani ya Mungu kwaajili yetu alipofufuka na kuketi mkono wa kuume hakuna awezaye kukifunga(Ufunuo 3:7).

8.Tunashiriki jina lake, jina lake ni letu, lilivyo tuko hivyo, ufahamu huu ni muujiza! Amemfanya kichwa kwa kumpa jina kwaajili ya kanisa (Waefeso 1:20-23).

9.Ufalme wa Mungu unafukuza ufalme wa Ibilisi Yesu anapotangazwa, pepo bubu, kiziwi nk wanaondoka.

10. Waliposema Neno, Mungu akashuhudia kwa matendo ya Roho Mtakatifu (Waebrania 2:1-3). Walienda kuhubiri kotekote, Bwana akaenenda pamoja nao na kulithibitisha lile Neno, Marko 16:20. Alienenda nao kwakuwa yupo hai.

No comments:

Post a Comment