Mtumie Yesu Kushinda Yote
Wakati wote
upitiapo hali yeyote ya kushindana kibinadamu au kishetani, usisahau kutumia
Nafsi ya Yesu Kristo, ni msingi wa kushinda. Jaribu ulilonalo ikiwa ni
nyumbani, katika huduma au kazini limekuja ili ushinde si uangamie. Watu
na Shetani watakuhukumu kwa yale unayopitia na kuona umeshindwa kwa vile
waonavyo wao, lakini mwisho utaongea na kuonyesha kushinda kwako!
YESU NI NANI
Yesu ni Kristo
Mwana wa Mungu aliye hai (Mathayo
16:16). Maneno haya alisema Petro,
Akiitija nafsi ya Yesu. Yesu alimjibu
kwa kusema, “Nami nakuambia wewe ndiwe
Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu wala milango ya kuzimu
haitalishinda” (Msitari wa 18).
Milango ya kuzimu haiwezi kuishinda nafsi ya Yesu Kristo. Mashauri yote ya kishetani hayawezi
kuishinda. Nyakati za Biblia milangoni
palikua ni sehemu ya mipango ya miji na mashauri (Kumbukumbu 16:18, 21:19,
Waamuzi 9:35). Baadaye mabaraza ya wazee
waliokuwa wakikaa milangoni na kufanya mashauri na yenyewe pia yaliitwa
milango. Kwa hiyo milango ya kuzimu
yaweza kumaanisha mashauri yote, mikakati yote ya kishetani, na hila zote. Hizi haziwezi kushinda nafsi ya Kristo Mwana
wa Mungu aliye hai.
MANENO YAONYESHAYO NAFSI YA YESU
Usomapo
maandiko hasa Injili nne, tafuta maandiko ambayo Yesu alijitambulisha nafsi
yake, Kwa mfano “mimi ndimi…” au “ Ajae
kwangu ….” “… Yangu” Maneno hayo yanamtambulisha Nafsi yake ikoje, yeye ni nani
na ana nini. Katika hayo Shetani hana
kitu wala mashauri yake ya kuzimu. Unapoombea
hali fulani kishetani simama katika kweli, Nafsi ya Kristo Yesu, utamiliki na
kushinda, mtaje Yesu ni nani katika tatizo hilo.
YESU ALIFANYA NINI MSALABANI?
Katika
Wakolosai 2:15, maandiko yanasema Yesu msalabani alizivua enzi na mamlaka.
Kuzivua kwa tafsiri ya Kiyunani ni “Katargeo”, maana yake ni; kuzifanya sio kitu,
kuzifanya sifuri,kuzipoozesha na kuzinyang’anya silaha. Utendaji wowote wa kishetani katika mawazo, hali
zinazokuzunguka, ua watu haziwezi kushinda nafsi ya Kristo aitwaye Yesu aliye
ndani yako. Msalaba umefanya hayo yote yaliyo
ya shetani kuwa si kitu.
YESU ALIISHIJE DUNIANI
Yesu aliishije
duniani? Aliishi kwa kushinda,
alishinda kila hila ya Shetani. Maandiko
yanasema alijaribiwa katika mambo yote bila kufanya dhambi!(Waebrania
4:15). Shetani alimjaribu katika mawazo
yake, hali, na kupitia watu, Yesu hakutenda dhambi.
Adamu na Eva
walishindwa kwa tamaa ya mwili, tamaa ya macho na kiburi cha uzima (Mwanzo
3:1-8). Yesu aliushinda ulimwengu
(Yohana 16:33). Aliushinda na mambo
yaliyo ndani yake, yaani tamaa ya mwili tamaaya macho na kiburi cha uzima
(1Yohana 2:13-17).
Hii (Tamaaya
mwili, tamaa ya macho na kuburi cha uzima).
Ni milango ya hila za kishetani kwenye maisha ya binadamu, Yesu alizishinda
pale mlimani wakati wa maombi ya siku arobaini.
Eva na Adamu walishindwa.
Katika nafsi
ya Yesu tunashinda sasa,Yesu ndiye tafsiri ya kweli katika yote tukutanayo
nayo. Katika yote yanayotutokea, ukweli
ni Yesu ni nani katika hali hizo, alifanya nini msalabani na aliishije
duniani na kushinda. Katika hali tukutanazo
nazo tuitaje Nafsi ya Kristo na neema ya kushinda uongo itatokea. Hata kama unaona unakufa huo ni uongo, ukweli
ni Yesu ufufuo na uzima (Yohana 11:25).
Hata kama unaona unashindwa ni uongo, ukweli ni kwamba Yesu aliye ndani
yako ameshinda ulimwengu na yote yaliyopo ndani yake (Yohana 16:33).
Kipaumbele chako wakati wote ukisahau
vitu vyote, Usimsahau Yesu ni nani, aliishije duniani, alifanya nini msalabani,
kisha mtaje katika mazingira yako. Ukifanya hivyo Yesu atasimama kama Kuhani
wako mbinguni kwa yele uyasemayo duniani.
No comments:
Post a Comment