Thursday, December 11, 2014

Tunampinga kwa Nafsi ya Yesu

MAANDIKO YANASEMA TUMTII MUNGU, TUMPINGE SHETANI NAYE ATAKIMBIA (YAKOBO 4:7). TUNAMPINGA ADUI SHETANI KWA NJIA YA YESU KRISTO.
MIFANO JINSI UWEZAVYO KUMPINGA:
1. Kwa Kristo Yesu aliye nuru, niliyejitiisha kwake kwa njia ya kumwamini, napinga giza katika ufahamu wangu, nuru ya hekima na ufahamu inaangaza ndani yangu siku ya leo.
2.Kwa Kristo Yesu aliye Uzima, napinga utendaji wa mauti wowote uliopangwa kinyume na mimi, Uzima wa Yesu unashinda maishani mwangu.
3.Kwa sura ya Kristo aliye mwema napinga sura ya Shetani aliye mwovu. Kila uonekano wa Shetani kama magonjwa, uchawi, ajali na uharibifu wowote, naupinga kwa sura ya wema wako.
4. Sema: Kwa njia ya Yesu aliye ndani yangu Shetani hana kitu kwangu (Yohana 14:30). Napinga ushetani wowote, kwa uungu wa Yesu, ulio pamoja nami.

LEO MTAMKE YESU JINSI YEYOTE UNAVYOMJUA ALIVYO, KATIKA HAYO MATAMSHI NA TABIA ZA YESU, MPINGE SHETANI.

No comments:

Post a Comment