Utoshelevu Wetu ni Yeye
Mungu ametutosheleza kuwa
wahudumu katika Agano jipya. Huduma ni utekelezaji wa kusudi fulani
linalofanyika ndani ya Yesu kwa uwezo wa Roho wake, ili kujaza pengo fulani, au
kutatua tatizo fulani. Kwa mfano kufanya kazi na kutoa sehemu ya mapato yako,
kuwafikia wasiofikiwa na injili, hiyo ni huduma, umetatua tatizo kwa sehemu la
kutofikiwa na injili. Hiyo kazi yako au
biashara ione kama ni huduma. Iombee ikirie Neno kama anavyoomba muhubiri kabla
ya kufanya huduma yake ya kuhubiri.
Unapofundisha Neno, unatatua
tatizo la watu kutojua Neno, hapo unahudumu. Unapofanya maombezi unaziba pengo
la watu kutolindwa au kutokuwa na neema ya kutimiza huduma zao hapo unafanya
huduma. Unaposhuhudia watu waokoke, unaziba pengo, unatatua tatizo la watu
kwenda jehanam. Unapotembelea mtu mwenye shida unatatua tatizo la kukata tamaa
nk! Unaposifu na kuabudu, unajaza pengo lisilojaa milele! La moyo wa Mungu
kutaka kusifiwa na kuabudiwa, hapo unahudumu.
Katika huduma yoyote ufanyayo
utoshelevu, au uwezesho wa kuweza kuitimiza sio wa kwako, bali watoka kwa
Bwana. Kwa njia ya Roho wake wewe ni muhudumu wa Agano jipya. Hutumii nguvu
zako na Sheria ya Musa bali nguvu za Roho. Katika huduma au tatizo lolote uliloumbwa
katika Yesu ulitatue kumbumka utoshelevu wako watoka kwake, sema hivyo, ombea
huduma hivyo. Maandiko yaliyofafanuliwa yanasema:
“Ni Yeye Bwana aliyetufanya tustahili na tuweze, kama wahudumu wa Agano
Jipya, Sio wa andiko la sheria, kwali kwa Roho Mtakatifu anayehuisha.” (2Wakorintho
3:6)
No comments:
Post a Comment