Monday, December 8, 2014

Shukuru kama Paulo



SHUKRANI ZA KANISA

Maandiko yanaonyesha shukrani alizoshukuru Paulo. Shukrani hizi  zinaweza kuleta ongezeko katika kanisa na maisha tunapozitumia. Kwa kushukuru namna hii tutakuwa tunafanya mapenzi ya Mungu, Maana shukrani ni mapenzi ya Mungu. Yesu alisema tuombe mapenzi yake yatimizwe. Shukrani hizi lazima zidhihirike, maana ni mapenzi ya Mungu.

1.    Alishukuru kwakuwa Warumi Walikuwa watenda dhambi wakatii Neema. Warumi 6:17 – 18 “ Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake; (18) na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki.” Unaweza  sasa ukamshukuru Mungu kwaajili ya kanisa au kwaajili yako kwamba ulikuwa mtenda dhambi lakini sasa umeitii neema.

2.    Shukuru imani yao inahubiriwa dunia yote. Warumi 1:8 “Kwanza namshukuru Mungu wangu katika Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa kuwa imani yenu inahubiriwa katika dunia nzima.” Unaweza kushukuru kwaajili ya imani yako ya wokovu, inahubiriwa, au inaweza kuhubiriwa duniani pote.

3.    Anatushangiliza daima. 2Wakorintho 2:14 “Ila Mungu ashukuriwe, anayetushangiliza daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu.”
4.    Anatutia bidii. 2Wakorintho 8:16 “Lakini ahimidiwe Mungu atiaye bidii ile ile kwa ajili yenu katika moyo wa Tito.”  Shukuru kwakuwa Mungu anakushangiliza daima. Katika hali zote zinazotokea unashangilizwa.

5.    Wanalipokea Neno linatenda kazi. 1Wathesalonike 2:13 “Kwa sababu hiyo sisi nasi twamshukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa, mlipopata ileneno la ujumbe la Mungu amlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neon la wanadamu, bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kweli kweli, litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini.” Shukuru kwakuwa Neno la Mungu unalolipokea linatenda kazi. Ikiwa wewe ni muhudumu wa Neno shukuru kwa Neno unalosema kwa watu wako kwamba linatenda kazi.

6.    Mungu amewachagua tangu mwanzo wapate wokovu katika kutakaswa na Roho. 2Wathesalonike 2:13 “ Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, ndugu mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokovu, katika kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli.” Shukuru kwaajili yako na kanisa kwamba Mungu amewachaagua tangu mwanzo, mpate wokovu katika kutakaswa na Roho.

7.    Omba na kushukuru  kwa macho ya kiroho  kufunguka na kuelewa mambo ya kiroho. Waefeso 1:15 – 23 “ Kwa sababu hiyo mimi nami, tangu nilipopata habari za imani yenu katika Bwana Yesu, na pendo lenu kwa watakatifu wote, (16)siachi kutoa shukrani kwa ajili yenu; nikiwakumbuka katika sala zangu, (17)Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye; (18)macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo; (19)na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake; (20)aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; (21)juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humutu, bali katika ule ujao pia; (22)akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo (23)ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.

No comments:

Post a Comment