Friday, December 19, 2014

Mshinde Aliye Mkuu

MKUU ALIYE NYUMA YA TABIA AU HALI
Katika hali mbaya unayopitia, au tabia ya mtu, nyuma yake kuna mkuu wa hali hiyo. Kwa mfano, mtu akiwa na jipu, kuna kiini chake, kisipotoka jipu haliishi, kiini hi hi ndicho mkuu wa jipu.

Unapoona kichuguu cha mchwa, yupo malkia, ukitaka mchwa watoweke, mtiweshe kwanza malkia, yeye ni mkuu wa mchwa hao.

Yesu alisema:"Hawezi mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu, na kuviteka vitu vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu; ndipo atakapoiteka nyumba yake" (Marko 3:27).

Unapoona mtu anatabia fulani kwa mfano, ana woga uliopiiliza, Woga huo ni kitu cha nje, nyuma yake kuna kiini. Unapomshauri shughulikia kiini yani roho ya woga.
Kunapokuwa na hali kwa mfano kila saa Tatu usiku unagombana na mtoto wako! Inawezekana kabisa kiini chake ni pepo aliyewekwa atende kazi wakati huo.
SHUGHULIKIA KITU HALISI, USISHUGHULIKIE KIVULI.

No comments:

Post a Comment