AMENIFIDIA
“Kwa maana Mwana wa
Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi”
(Marko 10:45)
Neno fidia katika andiko hili kama lilivyotafsiriwa toka
tafsiri ya awali ya Kiyunani ni, “lutron”.
Maana yake ni malipo ya ukombozi. Kwa
mfano zamani, baadhi ya watumwa walifanyika
watumwa kutokana na madeni waliodaiwa.
Akitokea mtu akalipa deni lile na mtumwa akawa huru kile kile
kilicholipwa hufidia maisha ya mtu huyo awe huru. Uhuru wa namna hii huitwa ukombozi au kununuliwa.
Maandiko yanaposema Yesu, alikuja awe fidia ya wengi kwa nafsi yake maana yake
ni awalipie mambo yaliyowafunga waachwe huru. Alitolewa na kujitoa mwenyewe
kama sadaka ilitukombolewe.
Sasa yupo mbinguni kama kuhani,
aliye shahidi wa sadaka aliyotoa mbele za Mungu. Tuwapo duniani tuyashike
maungamo yetu ya imani, na kuisema kazi yake ya ukombozi katika maisha Yesu;
bila shaka na yeye atasema mbinguni badala yetu( Waebrania 3:1, 4:14). Hatimaye
tutaona udhihirisho wa ukombozi duniani.
Sema Mbele za Yesu
Isimamishe imani yako katika ukombozi wa Yesu, unapoamini
ukombozi wake sema, hiyo ni roho ya imani husema (2Wakorintho 4:13).
I. Amenikomboa na Kifo
Sema: Kwa kifo chako Yesu sitakufa milele. Sitapotea katika ziwa la moto. Umenifidia
kifo change kwa kifo chako. Nakupa maisha yangu yote (Hosea 13:14, 1Wakorintho
15:51-58).
2. Amenikomboa na
Magonjwa
Sema: Kwa kupigwa kwako nimeponywa magonjwa. Gharama ya uzima
wangu uliilipa kwa kupigwa kwako. (1Petro 2:23-24).
3. Amenikomboa na
Uadui na Mungu
Sema: Adhabu ya amani yangu na Mungu ilikuwa juu ya Yesu,
nimeponywa mimi na Mungu sasa ni marafiki, amefanya amani kati yetu kwa damu ya
msalaba wake (Isaya 53:5, Wakolosai 1:20).
4. Amenikomboa na
Utumwa wa Ibilisi
Sema: Kwa sababu ya dhambi nilikuwa mtumwa wa dhambi na
Ibilisi. Yesu alikuja kuziondoa dhambi,
hivo Shetani hana kitu cha kunishikia yaani dhambi (1Yohana 3:7-8). Alikuwa
dhambi zangu niwe haki yake.
5. Amenikomboa na
Kukataliwa na Kuonewa
Sema: Nijapokataliwa na kuonewa Yesu alionewa na kukataliwa
na watu. Amenikomboa na kuonewa na kukataliwa hakutaniangamiza (Isaya 53:3).
6. Amenikomboa na
Umaskini
Sema: Yesu amenilipia
umaskini wangu kwa Yeye kuwa maskini.
Amefanyika umaskini wangu ili nipate utajiri wake (2Wakorintho 8:9).
7. Nimekufa na Kufufuka
Naye, na Kuketi Naye
Sema: Yesu ulipokufa nilikufa pamoja nawe katika dhambi,
ulipofufuka nilifufuka nawe katika haki, ulipoketi mkono wa kuhuume nimeketi
nawe, juu ya majina yote, mwenye jina kuu kuliko yote Wafilipi 2:9-11, Waefeso
1:21, Waefeso 2:5-6).
No comments:
Post a Comment