IMANUEL
(Mathayo 1:23)
Kusudi la mtu au mwisho wake ,
au mustakbali wake unaweza kuonekana kwa
vitu visivyopungua viwili
1.Unabii Ulionenwa juu yake
2.Jina lake au majina yake
Jina la Imanueli ambalo pia ni
jina la Yesu laonyesha kusudi moja la Yesu alilokuja kutimiza duniani. Andiko
hilo hapo juu linasema, ataitwa Imanueli yaani Mungu pamoja na wanadamu. Kuja
kwa Yesu ni mlango wa Mungu kukaa na wanadamu.
A. Anakaa Nasi kwa Njia ya kuzishika Amri Zake(Yohana 14:21,23)
1. Kuliamini jina la Yesu
(1Yohana 3:23): Amri hii ya kuliamini jina lake, tunaanza kuitii tunapompokea
Yesu kama Mwokozi. Tumapoitii Yesu anaanza kukaa nasi kwa uzima wake (1Yohana
5:13).
2.Kupendana sisi kwa sisi
(1Yohana 3:23).
B. Anakaa Nasi kwa Roho wake Mtakatifu (1 Yohana 3:24)
Roho Mtakatifu ni chanzo cha
makao ya Mungu pamoja nasi. Miili yetu ni hekalu la Mungu kwa njia ya Roho
Mtakatifu (1Wakorintho 3:16, 6:19-20). Mungu anasema atakaa ndani yetu na kati
yetu atatembea (2 Wakorintho 6:16). Siku ya leo wakati ninaomba nilipata
ushuhuda moyoni usemao, “Roho Mtakatifu ni Imanueli”. Yesu ni Imanueli, Roho
pia analo jina hilo maana ni mmoja na Yesu.
C. Anakaa Nasi Mkono wa Kuume (Waefeso 2:5-6)
Yesu ni Mungu pamoja nasi mkono
wa kuume wa Mungu. Yuko pamoja nasi juu ya kila jina, nguvu au mamlaka. Tunamwakilisha
duniani toka mkono wa kuume mbinguni. Mkono wa kuume tunatawaka pamoja naye
kama wafalme na makuhani. Tuko pamoja naye kama kuhani wetu na mwombezi wetu.
D. Atakaa Nasi Milele (Ufunuo 21:3)
Mungu atafanya maskani yake na
sisi milele. Yeye atakuwa ni hekalu na
sisi tutakuwa ni watu wake tulio ndani yake.
JINA LA IMMANUEL NI JINA LA KINABII
LA MUNGU KUKAA NASI. MUNGU ANAPENDA KUKAA
NA WATU, ANAKAA NASI KWA NJIA YA YESU KRISTO, IMMANUEL MUNGU PAMOJA NA
WANADAMU. HAPA NINAPOANDIKA IKIWA UMEMPA YESU MAISHA YAKO MUNGU YUPO NA WEWE!
UNAYO ROHO YAKE, UZIMA WAKE NA SAUTI YAKE KATIKA UFAHAMU WA ROHONI. KATIKA
KIPINDI HIKI MSHUKURU MUNGU KWA KUKAA NA WEWE KWA NJIA YA YESU.
No comments:
Post a Comment