Thursday, November 6, 2014

Umewezeshwa Kuwa Mwana


Kufanywa Mwana
Kwa kuwa hamkupokea tena roho ya utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia Aba, yaani Baba.” (Warumi 8:15).

Wala si hivyo tu; ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho, sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukikutazamia kufanywa wana yaani, ukombozi wa mwili wetu.” (Warumi  8:23).

Nyakati za Warumi na Wayunani, ikiwa mtu hakubahatika kupata mtoto, aliruhusiwa kuwa na mtoto ambaye sio wake kwa asili, ALIYEFANYWA MWANA, kwa kwa hatua na taratibu maalum. Mtoto huyo alitumia jina la baba huyu mpya kama baba yake kabisa na alikuwa na haki ya kurithi mali zake. Kitendo hiki cha kufanywa mwana kilikuwa na ngazi kuu mbili:
1. Kutambulika mwana binafsi
2.Kutambulika mwana katika jamii

KUTAMBULIKA BINAFSI
Hapa mtoto huyu mpya aliweza kuingia katika familia na kufanywa mwana halali. Alijulikana katika familia husika kama mwana na mrithi. Mwandishi wa Warumi alikuwa na maana hii katika andiko lifuatalo, “Kwa kuwa hamkupokea tena roho ya utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia Aba yaani Baba.” (Warumi 8.15). Sisi pia, Tulifanywa wana katika familia ya Mungu baba tukiwa hapa duniani, si wana tu tumefanywa warithi wake kwa njia ya Yesu, tunarithi vyote alivyorithi Yesu baada ya kufufuka katika wafu; Jina, mamlaka, haki yake nk.
KUTAMBULIKA KATIKA JAMII
Baada  ya kujulikana katika familia mtoto huyu, alitangazwa wazi katika jamii.  Hapa alitangazwa kwa uwazi zaidi. Andiko hili lifuatalo ndilo mwandishi alikuwa ana maana  hii,  Wala si hivyo tu; ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho, sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukikutazamia kufanywa wana yaani, ukombozi wa mwili wetu.” (Warumi  8:23).  Hata sisi, Siku moja tutaonekana wazi katika ufalme wa Mungu tutakapotambulishwa na Mungu mbinguni, baada ya miili yetu kubadilishwa na kuwa kama Yesu, tutaurithi uzima wa milele.

IKIWA UMEMPOKEA YESU, WEWE UMEFANYIKA MTOTO WA MUNGU. HUKUWA MTOTO ILA KWA NJIA YA YESU UMEFANYIKA MTOTO. UMERITHI YOTE ALIYORITHISHWA YESU BAADA YA KUFUFUKA. SASA UNASUBIRI KUTAMBULISHWA MBINGUNI KATIKA UFUFUO WA MILELE. USIKATE TAMAA, ICHUCHUMILIE SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment