KWA NJIA YA YESU
Katika maisha, utakutana na mambo ya kukandamiza na kukufanya usisogee mbele au usipande juu. Somo hili linakusaidia kuendelea kukaa juu. Ni somo la kuendelea kushika nafasi yako,ambayo adui anataka kukunyang'anya. Wako wanaotaka ukae chini, usifike mwisho, "maintain spirit of war."
ENDELEA KUWA JUU KWA KUFANYA MAMBO YAFUATAYO:
1. Usitafsiri Mambo Kama Yanavyoonekana(2Wakorintho 5:1-7)
Shetani alimpata Adam na Eva kwa kutazama tunda(Mwanzo 3:6)
Aliwapata Waizraeli kwa kutazama majitu na kujitazama (Hesabu 13:32-33)
Alitaka kumpata Yesu kwa kutazama jiwe life mkate nk (Mathayo 4:8).
WOTE WALIPASWA KUTAFSIRI HALI ZAO KAMA NENO LISEMAVYO, YESU ALIFANYA HIVYO.
Kwa mfano unasikia vitu vinakutembea, au kichwa kinauma kitu cha kwanza kujiuliza, "Neno linasemaje?"
2. Kaa katika Roho Mtakatifu.
Fanya kitu cha kiroho, kitakachoiachilia roho yako ishinde, maana inako kushinda kwa Yesu.
Litende Neno (Yohana 6:63)
Imba (Waefeso 5:19-20)
Nena kwa lugha(1Wakorintho 14:2)
Fanya Kama Yesu kwa yale unayokabiliana nayo-jiulize, angekuwa Yesu angefanyaje hapa? Utakachofanya ni kuenenda kwa roho (Wagalatia 5:25).
3.Mtamke Yesu (Luka 10:18-20)
Baada ya mitume kumtangaza Yesu, Shetani alianguka kama radi.
Upako ni Yesu ndani yako, ukimtamka anaachiliwa kwa nguvu.
4.Shambulia Jina la Shetani
Tabia ya Shetani kwako inajifunua kwa jina Lake:
A. Shetani (Mpinzani)
B.Ibilisi (Mshitaki-devil)-Ufunuo 12:9
C.Abadon (muaribifu)-Ufunuo 9:11
D.Mwizi-Yohana 10:10.
Litaje jina lake na kusema, kazi zake zinazo onekana kwa jina lake hazitasimama.
6.Kaa katika Agano
Mahusiano na Mungu kama mwana Wake.
Ushirika na Mungu wa kila siku
Haya yanawezekana kwa damu ya Yesu, kifungo cha Agano. Mahusiano yako na Mungu na ushirika katika damu hayana mwisho.
Yohana 6:37
Yohana 10:38
Mathayo 26:25-27
No comments:
Post a Comment