HAKI YANGU KATIKA KRISTO
"Twajua ya kuwa kila aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; Bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi" (1 Yohana 5:18).
1.UMEZALIWA NA MUNGU
Kuzaliwa na Mungu ni kuunganishwa na Yesu (1Wakorintho 5:17-18). Kabla ya kuunganishwa na Yesu ulikuwa umeunganishwa na Adamu ukapata mauti. Baada ya kutubu na kuiweka imani yako kwa Yesu, umezaliwa na Yesu na kupata uzima wa milele.
2.HUTENDI DHAMBI
Asili yako baada ya kuzaliwa na Mungu si dhambi ni haki. Usijione ni mwenye dhambi katika Adamu, jione mwenye haki katika Yesu. Ni kweli kuna jaribu la dhambi kwasababu ya mwili, lakini unao uwezo wa kushinda, maana roho yako ina asili ya mbinguni. Kujiona una dhambi si unyenyekevu ni kutojua kuwa Yesu alifanyika dhambi zako. Hata hivyo usitende dhambi makusudi kwa kuwa una haki! Huko ni kuidharau kazi ya msalaba. Ikiwa baada ya kuamini umetenda dhambi, tubu haraka (1Yohana 2:1-2).
3.UNALINDWA
Andiko lililotajwa hapo juu, sehemu inayosema aliyezaliwa na Mungu hujilinda, tafsiri yake katika Biblia iliyofafanuliwa ni "hulindwa". Ikiwa umempa Yesu maisha yako unalindwa! Haufanyi chochote ili ulindwe, upo katika agano la ulinzi, kwa kuwa umezaliwa na Mungu.
4. HAUGUSWI!
Shetani hakugusi! Ikiwa umezaliwa mara ya pili na kudumu kuwa na Yesu Shetani hakugusi.
ANZA KUFIKIRI NA KUSEMA HIVYO, UTAISHI KATIKA ROHO NA NEEMA YA NENO HILI, KAMA BADO HUJAZALIWA NA MUNGU KUPITIA YESU SEMA: MUNGU, NISAMEHE DHAMBI KWA NJIA YA YESU. YESU NAKUSHIKA SASA, NAIWEKA IMANI YANGU KWAKO. NAAMINI KWA NJIA YAKO MUNGU ANANIKUBALI KAMA MWENYE HAKI. YESU ULIKUFA NA KUFUFUKA WEWE NI BWANA!
No comments:
Post a Comment