Thursday, November 13, 2014

Mpinge Kwenye Jina

JITIISHE KWA NENO, PINGA KWA NENO
Maandiko yanausema mtiini Mungu mpingeni Shetani, Naye atakimbia(Yakobo 4:7) Shetani haondoki kwa kumtazama na kuogopa au kulalamika kwamba ni mbaya. FANYA KITU MBELE ZAKE MPINGE .

Kabla andiko hili halijasema tumtii Mungu, msitari wa sita unaonyesha kuwa unyenyekevu huleta neema. Kutii ni ishara ya kunyenyekea, kujishusha. Kingereza inasema "submit" yaani jishushe, hasa chini ya mwenye mamlaka.

Tunamtii Mungu kwa njia ya kujishusha, kujinyenyekeza chini ya mamlaka yake. Mamlaka yake kuu ni Neno na Roho Mtakatifu. Tujiwekapo chini ya Neno lake na Roho wake, tayari tunao uwezo wa kumpinga Shetani. Maandiko yanasema atakimbia!
                                    
   JINSI YA KUMPINGA
Tunapokutana na mazingira ya kishetani yanayotisha. Tunaanza kumpinga katika jina lake. Jina lake Shetani laonyesha mwisho wake na utendaji, pia jinsi alivyo.
                  IBILISI AITWAYE SHETANI
A.IBILISI
Majina haya mawili Ibilisi na Shetani yanatofauti. Ibilisi (devil) ni mchonganishi, mshitaki. Ni mchongezi, anatenda kazi kwa namna ya kukuchonganisha na Mungu. Alipomfuata Adamu na Eva aliwafuata kama Ibilisi akimshitaki Mungu na kusema, Mungu anajua wakila tunda watakuwa kama Yeye.
Alipomfuata Mungu kwaajili ya Ayubu alimchongea kwa kusema Mungu akimgusa Ayubu, Ayubu atamkufuru.  Alisingizia kwamba Ayubu  alimcha Mungu kwasababu tu, Mungu amemfanyia kitu fulani.
B.SHETANI
Shetani (Satan) maana yake ni mpingamizi. Anapinga kila kitu chema. Yupo kinyume na uhai wako, amani yako afya yako, uchumi wako, watoto wako nk.  Kama unaona, anataka macho yako yasione, uwe kipofu au utazame picha chafu.

Kama unatembea anataka uwe kilema, kama unasoma anataka uache shule. Zaidi ya yote anataka usimpate Yesu upotee milele Jehanam. Hiyo ndiyo maana ya Shetani, ni mpingamizi wako, SIYO RAFIKI YAKO!
                 ANZA KUMPINGA JINA LAKE
Jina linabeba tabia na nguvu ya mwenye nalo. Jina la Ibilisi na Shetani ndio linaneba kazi na tabia zake zilizo kinyume na maisha yako. 
Mtii Mungu kwa kujitiisha chini ya Neno lake.  Kisha anza kumpinga Shetani kwa Neno,  kwa kutamka neno la Mungu kinyume na jina lake.

Sema: NAIPINGA NAFSI YAKO SHETANI KATIKA MAISHA YANGU KWA NAFSI YA YESU KRISTO. WEWE NI IBILISI MSHITAKI, NAKUPINGA KWA NENO LA KRISTO LISEMALO YEYE NI MPATANISHI.
TABIA ZAKO ZOTE ZA UHARIBIFU ENEO LOLOTE LA MAISHA YANGU, ZILIZOBEBWA NA JINA LAKO SHETANI, HALI ZOTE ZA UPINGAMIZI, NAZIPINGA KWA YESU KRISTO, ALIYEKUJA NIWE NA UZIMA KISHA NIWE NAO TELE.  NALIPINGA JINA LAKO IBILISI KATIKA MAWAZO YANGU. HUTANIDANGANYA KWA HILA. HUTANISHITAKI KATIKA NAFSI YANGU NA KUNIFANYA NIJIHUKUMU. KAZI ZOTE ZA KIIBILISI NA KISHETANI KATIKA MAISHA YANGU NAZIPINGA KWA YESU KRISTO MWOKOZI WANGU.

No comments:

Post a Comment