UMELIPIWA
"Basi Yeye atufanyaye imara pamoja nanyi katika Kristo, na kututia mafuta, ni Mungu, naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu" (2Wakorintho 1:22-23).
Tulipompokea Yesu kama Mwokozi, tulizaliwa mara ya pili kwa Roho Mtakatifu
(Yohana 3:6).
Kitendo cha kuzaliwa na Roho Mtakatifu, kimeambatana na kitendo cha kufanywa wana wa Mungu (Warumi 8:17-24). Hatukuwa wana tumepewa roho ya kufanywa wana kwa Roho Mtakatifu.
Katika Roho huyo tumetiwa muhuri kama alama ya kuwa sisi ni mali ya Mungu. Tunaenda mbinguni kuurithi Uzima wa milele. Hakikisho, ambalo latuonyesha kuwa siku moja tutaurithi Uzima wa milele ni ARABUNI ya Roho.
Arabuni ni malipo ya kwanza yanayothibitisha kuwa siku moja utalipa yote. Kwa mfano ukienda dukani na kukuta kiatu kinauzwa elfu hamsini. Ukaamua kutoa elfu ishirini na thelathini kumalizia baadaye, elfu ishirini hiyo uliyotoa ni arabuni. Inakupa umiliki wa kiatu na kutoa hakisho kuwa siku moja utalipa malipo yote. Pia soma Waefeso 1:13-14.
IKIWA UMEZALIWA KATIKA YESU, KWA ROHO MTAKATIFU UMELIPIWA MALIPO YA KWANZA, UNALO HAKIKISHO KWAMBA SIKU MOJA UTAURITHI UZIMA WA MILELE. HAKIKISHO HILO NI ROHO MTAKATIFU ALIYE NDANI YAKO. UNAYO ARABUNI YA ROHO. MTII KWA KUISHI KWA TUNDA LA ROHO, ONGEA NAYE NA KUJIWEKA WAKFU CHINI YAKE. UKITAKA KUINGIA MBINGUNI KAA KARIBU NA ROHO MTAKATIFU. AMETUMWA KUHAKIKISHA UMEURITHI UZIMA WA MILELE.
No comments:
Post a Comment