Monday, October 27, 2014

Roho wa Uzima

YESU ANAHUISHA YOTE YALIYOKUFA

Adam wa mwisho ni Roho mwenye kuhuisha, Anaondoa mauti. Palipo na giza anahuisha na kuleta nuru. Palipo na dhambi anahuisha na kuleta utakatifu. Palipo na uongo anahuisha na kuleta kweli (1Wakorintho 15:45).

 Mwili wa Adam uliolala kama mavumbi, Mungu alipoupulizia pumzi ya uhai ilikuwa ni mfano wa roho ya Kristo. Mifupa ya Ezekiel 37, ni mfano wa roho ya Kristo. Roho ya Yesu inavifanya vitu viwe Hai. Yesu ni Pumzi inayofanya vitu viwe hai. Mungu aliposema nchi na ijawe na viumbe Hai (Mwanzo 1:24), bila shaka ilikuwa ni Roho ya Kristo.

  Yesu alipotoka katika mwili na kwenda kuzimu kuharibu dhambi na mauti, aliporudi duniani, mwili wake ukahuishwa ukawa mpya. Kifo kililetwa na Adamu ndio maana alikufa. Ufufuo umeletwa na Yesu, ndio maana amefufuka. Alikufa afanane na Adamu akafufuka tufanane naye(1 Wakorintho 15:35-49).

IKIWA YUPO NDANI YAKO SASA, KUMBUKA ANAFANYA HAI VILIVYOKUFA.

No comments:

Post a Comment