KUMWAMINI YESU NI KUMTEGEMEA YEYE ILI KUOKOLEWA. HAKUNA MTU ATAKAYEMWONA MUNGU IKIWA IMANI YAKE HAJAIWEKA KWA YESU. IKIWA UMEMWAMINI YESU, YAFUATAYO NI MATOKEO YAKE, UNAWEZA KUYATAMKA KWA UJASIRI.
1.Nimemwamini sitakufa katika dhambi (Yohana 8:24).
2.Nimemwamini sitakaa gizani (Yohana 12:44-46).
3.Nimemwamini mito ya maji (Roho wa Mungu) inatoka ndani yangu (Yonana 7:38-40).
4.Nimemwamini nimehesabiwa haki kwa imani (Warumi 10:10).
5.Nimemwamini nimeunganika na Yeye
(Warumi 11:23):
WANA WA ISRAELI KWA KUTOAMINI WALIKATWA TOKA MTI WAO WA ASILI(WARUMI 11:23). IMANI INATUUNGANISHA KATIKA MTI, YAANI YESU. INATUUNGANISHA NA MUNGU. TUMEPANDIKIZWA NDANI YA MUNGU KWA NJIA YA KUMWAMINI YESU. SISI NA BABA TU UMOJA, KATIKA YESU KRISTO TUNASHIRIKI UUNGU:
Tunashiriki jina lake
Tunashiriki kiti chake
Tunamshiriki Baba yake
Tunashiriki heshima yake
Tunashiriki Roho wake! Roho aliye ndani ya Mungu Baba yupo ndani yetu pia ni maajabu!
Tunaenda kushiriki Uzima wake milele na milele.
No comments:
Post a Comment