UTAONDOKAJE?
"Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; Bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele" (Mathayo 25:46).
Kuna mwisho wa namna mbili tu, kwa kila mwanadamu. Ikiwa umezaliwa na Adamu tu, wewe ni mwenye dhambi, mwisho wako ni katika adhabu ya milele.
Yakupasa uzaliwe tena na Yesu(Yohana 3:6). Unazaliwa naye kwa kumtegemea ili Mungu akukubali, yaani akuhesabie haki. Kumtegemea huku ni mfano wa mtu anayezama baharini, kisha akatupiwa boya, atalitegemea lile boya, ataliamini kwamba linaweza kumwokoa. Ndivyo ilivyo kwa Yesu, mwamini kwa maana ya kumtegemea kuokolewa na ziwa la moto, dhambi, dunia na matendo ya mwili.
Ikiwa umeshampa maisha yako mfuate. Uwe tayari kukosa chochote ila sio Yeye na maneno yake. Usichanganye maisha, huko ni kumdhihaki Mungu, Yeye yupo "serious" na mwisho wa maisha yako. Ujue maisha yako si mali yako ni yake Yesu (1 Wakorintho 6:19-20).
LENGO KUU LA KILA MTU LIWE KUIONA SURA YA MUNGU SIKU MOJA KWA NJIA YA YESU, NDIPO MENGINE YAFUATE.
Sema: Yesu nakutegemea kuzaliwa mbinguni. Nimezaliwa duniani kwa Adamu. Sasa nazaliwa mbinguni kwa wewe Yesu. Nioshe kwa damu yako, ingia ndani yangu sasa, NINAKUAMINI KUOKOLEWA MILELE.
No comments:
Post a Comment