INAWEZEKANA
Biblia ni kitabu cha ajabu! Kwa neema ya Mungu nimesoma sana Agano Jipya, lakini leo nimekutana na andiko ambalo utafikiri halikuwepo! nimepata Rhema, linasema, "wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto" (Mathayo 3:9).
Maneno haya alikuwa akiyasema Yohana mbatizaji kwa Mafarisayo na Masadukayo. Neno lililoushika moyo wangu ni: KUTOKA KATIKA MAWE YA MTO YORDANI MUNGU ALIKUWA ANAWEZA KUMPA IBRAHIMU WATOTO. TWAWEZA KUSEMA MUNGU ANA UWEZO KUGEUZA MAWE YAWE WATOTO!
Yohana hakusema kitu kwa bahati mbaya, alikuwa amejazwa Roho toka tumboni, alimaanisha alichosema katika uwezo wa Roho Mtakatifu.
Kama Mungu ana uwezo kugeuza mawe yawe watoto! Itakuwa vigumu kwake kumpa mtoto mwanamke ambaye hana kizazi! Au mwanamume aliye dhaifu maeneo ya uzazi. Kwa yeyote asiye na mtoto, Mungu awezaye kugeuza mawe yawe watoto, hashindwi na umri wako kuendelea sana au kupungukiwa katika maumbile ya uzazi. Anza kuwaza hivyo kuhusu Mungu wako,
ANAWEZA!
Hakika Anaweza....AMEN!!
ReplyDelete