Wednesday, October 15, 2014

Amri Mpya

KAINOS

Maandiko yanasema Yesu ametupa amri mpya, tafsiri yake ni amri iliyofanywa upya. Neno linaloonyesha kufanywa upya linaitwa KAINOS.

                   ZAMANI ILIKUWAJE?
"Usifanye kisasi wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako; Bali umpende jirani yako kama nafsi yako; mimi ndimi Bwana" (Mambo ya Walawi 19:18).
                                 
                        SASA IKOJE?
"Amri mpya nawapa, mpendane kama mimi nilivyowapenda ninyi mpendane vivyo hivyo" (Yohana 13:34).

                 YESU  ALITUPENDAJE?
Alijitoa akafa
Alijinyenyekeza akawa mtumwa

ZAMANI MUNGU ALISEMA TUWAPENDE JIRANI KAMA NAFSI ZETU. SASA KATIKA YESU AMRI HIYO IMEFANYWA UPYA(KAINOS), SASA TUNAPASWA KUWAPENDA JIRANI KAMA YESU ALIVYOTUPENDA. KIPIMO SI NAFSI ZETU SASA, BALI YESU KRISTO. KAMA ALIVYOJITOA KUTUTUMIKIA, KAMA ALIVYOJINYENYEKEZA KWAAJILI YETU; YATUPASA KUNYENYEKEANA NA KUTUMIKIANA (WAEFESO 5:21). TUKUBALI KUONA WENGINE WANAINUKA KWA KUWEPO KWETU, KUONA WAO WANAZIDI KABLA YA SISI, TUJIVIKE UPENDO UNAOJIFUNUA KWA KUNYENYEKEANA, HIYO NI NIA YA KRISTO (WAFILIPI 2:5-11, 1PETRO 5:5).

No comments:

Post a Comment