Monday, October 13, 2014

Maneno ya Ufahamu

WAKATI NINAOMBA NILIFAHAMU MANENO HAYA KATIKA ROHO YANGU
                               
Mwili wa Adam uliolala kama mavumbi, wakati wa uumbaji, Mungu alipoupulizia pumzi ya uhai ilikuwa ni mfano wa Roho ya Kristo. Ni Roho iletayo uhai.

Mifupa ya Ezekiel 37, ni mfano wa Roho ya Kristo. Ni pumzi inayofanya vitu viwe hai. Israeli ilifanywa hai kama Taifa kwa Roho ya Kristo.

Mungu aliposema nchi na ijawe na viumbe hai(Mwanzo 1:24), bila shaka ilikuwa ni Roho ya Kristo. Ikaleta uhai na ongezeko.

Yesu alipotoka katika mwili na kwenda kuzimu, aliporudi duniani, mwili wake ukahuishwa ukawa mpya. Kifo kililetwa na Adamu ndio maana alikufa. Ufufuo umeletwa na Yesu, ndio maana amefufuka. Alikufa afanane na Adamu kwaajili yetu akafufuka tufanane naye(1 Wakorintho 15:35-49).

ROHO YA YESU INAHUISHA, INAAMSHA, INAFANYA UPYA, INAREJESHA, INASIMAMISHA NA KUTEGEMEZA. AMINI UKIWA NA YESU UNA ROHO YAKE. HAPA SIZUNGUMZII ROHO MTAKATIFU, NAZUNGUMZIA 'UYESU' ULIO NDANI YAKO BAADA YA KUMWAMINI.

No comments:

Post a Comment