Friday, October 17, 2014

Shukrani Mapenzi ya Mungu

MAOMBI YETU YACHANGANYWE NA SHUKRANI

"Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani;" (Wakolosai 4:2).
"Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwaajili ya watu wote;" (1Timoteo 2:1).

YATUPASA KUOMBA KWA MAPENZI YA MUNGU
"Na Huu ndio ujasiri tulionao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawa sawa na mapenzi yake, atusikia" (1 Yohana 5:14).
Mtu akiomba kinyume na mapenzi ya Mungu hasikiwi maombi yake. Hii inaonyesha mtu anaweza kukosea kuomba ikiwa maombi yake yapo kinyume na mapenzi ya Mungu.

SHUKRANI NI MAPENZI YA MUNGU
Ashukuriwe Mungu, hakuna atoaye shukrani kwa Mungu akakosea, shukrani ni mapenzi ya Mungu,"Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu"(1Wathesalonike 5:18).

Kama hujui utafanyaje mapenzi ya Mungu katika maisha yako, anza kwa shukrani. Shukuru kwa jina la Yesu (Waefeso 5:20). Unaweza kuomba ukakosea, lakini huwezi kushukuru ukakosea.

CHANGANYA MAOMBI YAKO NA SHUKRANI. SHUKRANI NI MAPENZI YA MUNGU, MAOMBI YATUPASA KUYAFANYA KWA MAPENZI YA MUNGU. NAAMINI NDIO MAANA PAULO ALICHANGANYA MAOMBI YAKE NA SHUKRANI, PENGINE NI ILI YAWE NA MAPENZI YA MUNGU.

Unaposhukuru katika maombi, kwa kila jambo, unakaribisha mapenzi ya Mungu katika jambo hilo, hata kama ni baya. Ni kweli kuna mambo mabaya tunakutana nayo, Ila ni fursa kwetu katika hayo kufanya mapenzi ya Mungu, KUSHUKURU.

2 comments:

  1. BWANA YESU asifiwe sana mchungaji! Kwa muda mrefu nilikuwa najiuliza sana kwanini tushukuru kwa kila jambo, lakini mafundisho haya yamenifunulia sehemu mojawapo ya siri hiyo, kulifanya jambo la mwombaji libebe mapenzi ya MUNGU! Asante sana mwalimu, BWANA YESU akutangulie wakati wote!

    ReplyDelete
  2. Mungu akubariki Mchungaji kwa maana nyingine maombi yanayo jibiwa moja kwa moja ni ya shukurani,maana mambo mengine yanaweza yasijibiwe kwa sababu si mapenzi ya Mungu

    ReplyDelete