Sunday, September 14, 2014

Kupungua

HETTEMA
Tuliona maana ya neno HARMATIA ni kukosa shabaha, ikiwa na maana ya dhambi. Maana nyingine ya neno dhambi ni HETTEMA. Hii inabeba hali ya kupungua, au kupungukia kitu ambacho hakikupasa kupungukiwa. Ni kitu kupungua na kuonekana kutokamilika na kuwa na kasoro. Mfano mtu anaweza akawa anatembea lakini hana kidole cha mguu. Huyu amepungua, dhambi Ina sura hiyo ni upungufu, ni kasoro.
 Katika 1Wakorintho 6:7, imeandikwa,"Basi imekuwa upungufu kwenu kwenu kabisa kwamba mnashitakiana ninyi kwa ninyi..."
Kutenda dhambi ni kufanya jambo lililopungua katika kiwango ambacho Mungu alitegemea. Hapa utagundua Pia, hatuwezi kutopungua mbele za Mungu. Ni kwa njia ya Yesu tu tunaweza kuwa watimilifu. Utimilifu wako ni kwa njia ya Yesu uliyeweka imani yako kwake.
Maandiko yanasema, "Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi yote na mamlaka." (Wakolosai 2:10).

LEO OMBA MWAMBIE MUNGU ASANTE, KWA KUWA KATIKA KASORO ULIZONAZO,ZINAZOKUFANYA UPUNGUE KATIKA VIWANGO VYA HAKI YAKE YESU NDIYE UTIMILIFU WAKO, MBELE ZAKE MUNGU.

No comments:

Post a Comment