Saturday, September 13, 2014

Kukosa Shabaha

HARMARTIA
Moja ya tafsiri za neno dhambi ni: HARMARTIA. Maana yake yake ya msingi ni kukosa shabaha.
Katika Warumi 8:3, Yesu aliihukumu dhambi katika mwili wake. Mara zote tunakosa shabaha ya mapenzi ya Mungu tukiwa wenyewe, Bila Yesu.  Hiyo hali ya kukosa shabaha iliyo ndani yetu, yaani dhambi Yesu aliihukumu kwa mwili wake akaiua.
Hivyo tumtegemee Yeye kutufanya tusikose shabaha ya mapenzi ya Mungu. Tunapofanya juhudi kutotenda dhambi tumwone kwa imani Yesu yupo pembeni katushika. Kumtegemea Yesu au kumwamini ni nyenzo ya kutufanya tusikose shabaha.
Tunapotenda yote kwa njia ya Yesu, hatutakosa shabaha mbele za Mungu. Tutapiga shabaha katika mapenzi yake. Kumwamini Yesu ni dawa ya dhambi (Yohana 16:9).
Maandiko yanasema, "Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi." (Yakobo 4:17).
LEO MWOMBE MUNGU AKUCHUNGUZE MOYO WAKO NA KUKUONYESHA NI JAMBO GANI JEMA UNALIJUA NA HULIFANYI, AMBALO KWAKO LIMEKUFANYA UKOSE SHABAHA YA MAPENZI YA MUNGU. INAWEZEKANA NI MTU ILIKUPASA UMWOMBEE HUJAOMBA NK. MWOMBE MUNGU AKUPE NEEMA YA KUJUA JAMBO HILO NA KULITENDA, KWA NJIA YA KUMWAMINI AU KUMTEGEMEA YESU.

No comments:

Post a Comment