Monday, September 15, 2014

Dhambi za Kutojua

AGNOEEMA
"Lakini katika hema hiyo ya pili kuhani mkuu huingia peke yake, Mara moja kila mwaka; Wala si pasipo damu, atoayo kwaajili ya nafsi yake na kwa dhambi za kutojua za hao watu." (Waebrania 9:7).
Maana nyingine ya dhambi inatoka katika neno la Kiyunani, "AGNOEEMA". Maana hii inaendana na kutokujua jambo wakati ilikupasa kujua. Unaweza kutenda kosa au dhambi pasipo kujua, ingawa ilikupasa kujua.
Katika sheria za nchi kutokujua sheria hakukufanyi usihukumiwe ukikosea, eti kwa kuwa hukujua sheria imekataza jambo ulilofanya. Kwa maana hii ndio maana yatupasa kusoma neno la Mungu wakati wote, ili tujue sheria yake na kuitenda. Kwani kutenda dhambi kwa kutojua hakuifanyi isiwe dhambi, ilitupasa tuijue.
Ashukuriwe Mungu kwa kuwa tunaye Kuhani. Ukuhani wa Yesu Una nguvu ya kutuwezesha kuokolewa kutoka katika matokeo ya dhambi ya kutojua, na inayojulikana (1 Yohana 2:1-2). Hata hivyo yatupasa tujifunze maandiko ili tuijue dhambi na kujilinda.
LEO MSHUKURU MUNGU KWA KUHANI YESU. DHAMBI ZAKO ZA KUTOJUA, YEYE NI  MWOMBEZI AU WAKILI KWA AJILI YA DHAMBI HIZO,  PIA YEYE NI UPATANISHO. KATIKA YEYE TUNAWEZA KUWA NA AMANI NA MUNGU. HATA HIVYO YAKUPASA KUSOMA NENO SANA, ILI UJUE DHAMBI NA KUJILINDA NAYO. HII ITAKUWEZESHA KUTOFANYA DHAMBI YA KUTOJUA.

No comments:

Post a Comment