Tuesday, September 16, 2014

Kuanguka Wakati Ulipaswa Kusimama

PARAPTOMA
Dhambi maana yake nyingine ni kuanguka wakati ilikupasa kusimama. Dhambi ni kukosa shabaha, kupungua, Pia ni kuanguka.  PARAPTOMA ni neno lililotumika kwa maana hii, likimaanusha dhambi.
Waefeso 1:7, "Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawa sawa na wingi wa neema yake."
Bila shaka dhambi inayitajwa hapa ni ile Adamu aliyotenda bustani ya Edeni. Pale alikosea na akaanguka, wakati ilimpasa kusimama. Kwa dhambi hiyo ya Adamu wote tukawa na dhambi (Warumi 3:23).
Kwa damu ya Yesu tumekombolewa, tumenunuliwa toka katika utumwa wa dhambi ya Adamu (1 Petro 1:18-19).

Inatupasa kuendelea kusimama wakati tunajaribiwa kufanya dhambi. Udhaifu wa mwili ndio uletao anguko wakati wa majaribu. Yesu aliwaambia wanafunzi wakeshe waombe wasije kuingia majaribuni (Mathayo 26:41). Kuomba, kusoma Neno na kutenda mambo ya kiroho, kunaziwezesha roho zetu kuwa juu ya udhaifu wa mwili ambao hauwezi kushinda dhambi, hatimaye tunapojaribiwa tunaweza kushinda kwa roho zetu zenye ushirika wa karibu na Mungu.

Imeandikwa, "Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuliana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi." (Waebrania 4:15). Kundelea kusimama wakati tunajaribiwa tuanguke, kunawezeshwa na imani zetu kuziweka kwa Yesu aliyejaribiwa na hakuanguka katika dhambi.

SEMA MBELE ZA MUNGU, KWA NJIA YA YESU ALIYEJARIBIWA NA KUENDELEA KUSIMAMA, HUTAANGUKA, UTAENDELEA KUSIMAMA. PIA UWE NA NIDHAMU WAKATI WOTE KUKAA KIROHO, KUOMBA, KUIMBA, KUSOMA NENO, ILI KUSHINDA UDHAIFU WA MWILI KUTAKA DHAMBI.

No comments:

Post a Comment