Sunday, September 7, 2014

Kazi za Amani - III

VI. Umuhimu wa Amani
  1. Amani inaunganisha, “…Tukijitahidi kuuhifadhi umoja wa ROHO katika kifungo cha Amani” (Waefeso 4:3).

-Inaunganisha Ushirika
-Inaunganisha mtu na Mungu
-Inaunganisha moyo wa mtu uliogawanyika kwa vidonda

    1. Amani inashika Neema na Hekima
Neema
-Uwezo wa kiungu kutenda
Amani inapoushika moyo uwezesho wa neema kama kuweza kumsikia Mungu, kuweza kumtumikia kunafanikiwa

Hekima
-Namna ya kutenda
-Amani ikiwepo maelekezo ya kiungu moyoni huanza. Ni rahisi kupata hekima ya kutenda jambo ukiwa na amani
MOYO WENYE AMANI HUACHILIA NGUVU NA MBINU ZA KUITENDEA KAZI NGUVU HIYO.

    1. Kazi ya amani moyoni ni msingi wa mema yote.

VII. Funguo za Amani

TOBA
  1. Mwamini Yesu na kuitegemea kazi ya Msalaba ili usamehewe.
MAOMBI
  1. Baada ya kumkabidhi Mungu tatizo lako linalokusumbua endelea kutamka kama yeye analo usijisumbue (Wafilipi 2:6-7), utasema kama Daudi, “Katika amani nitajilaza na kupata usingizi, maana wewe Bwana peke yako ndiye unijaliaye kukaa salama” (Zaburi 4:8).
UWE NURUNI MBELE ZA MUNGU
  1. Usifiche dhambi kwa Mungu-Hapana amani kwa wabaya
NENO
  1. Kaa katika Neno, Yesu alitamka kwa wanafunzi “Amani iwe kwenu” Neno lake liliwapa amani” (Yohana 20:19). “Wana amani nyingi waipendao Sheria yako wala hakuna la kuwakwaza” (Zaburi 119:165). “Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia.” (Ayubu 22:21).
OMBA KWA ROHO
  1. Ukosapo amani katika uamuzi tumia muda kunena kwa lugha. Amani ikizidi kukosekana acha uamuzi huo (Wakolosai 3:15). Tunda la Roho (Wagalatia 5:22).

Amani na iwe kwa ndugu na pendo pamoja na imani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Bwana Yesu Kristo (Waefeso 6:23).

  DAMU
6.Sema kwa njia ya damu ya Yesu una amani na Mungu na dhamiri yako.

No comments:

Post a Comment