Saturday, September 6, 2014

KAZI YA AMANI - II




IV. Amani Kabla ya Anguko

Kabla ya Adamu kumkosea Mungu katika bustani ya Edeni alikuwa na amani na Mungu kwa sababu alikuwa na haki na uzima.
Adamu alipokosea alikuwa adui na Mungu-Amani hamna
Alikuwa anamashitaka katika dhamiri yake-Amani hamna

Kabla alikuwa na utulivu wa ndani, na kati yake na Mungu kwasababu ya kutokuwa na dhambi, Kazi ya haki ya Mungu ndani yake ilimpa amani, “Na kazi ya haki itakuwa amani. Na mazao ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima.” (Isaya 32:17).

Baada ya kumwasi Mungu Adamu alipoteza haki, hapohapo amani ikapotea, inaonekana kuwa amani ya ndani haikuwepo ndio maana alianza kujificha.

-Alipokosa haki ya Mungu kwa kuasi akawa mtu mbaya na hapana amani kwa wabaya. “Mimi nayaumba matunda ya midomo; amani, amani kwake yeye aliye mbali na kwake yeye aliye karibu. Bali wabaya wanafanana na bahari iliyochafuka; maana haiwezi kutulia. Hapana amani kwa wabaya; asema Mungu wangu.” (Isaya 57:19-21)

*Adhabu mojawapo aliyoipata Adamu baada ya kutenda dhambi ni kukosa amani.

V. Chanzo cha Amani

Yesu alikuja ili tuwe na utulivu wa ndani na kutokuwa na uadui kati yetu na Mungu.

Alikuja kuiondoa dhambi ya Adamu, iliyotufanya tusiwe na amani na Mungu

Pia alikuja kutoa damu yake dhamiri zetu zisafishwe tuwe na amani ndani yetu.

Jambo lingine alilofanya ni kubeba adhabu ya amani aliyoipata Adamu yaani kukosa amani.

“…Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.” (Isaya 53:5).

Pia unaweza kusoma (Waefeso 2:15-17).
-Kazi ya Yesu Msalabani imeleta amani na MUNGU
-Amani Katika mioyo
-Amani kati ya watu

Mtu anapotubu dhambi zake kupitia Yesu, na kuitegemea kazi ya msalaba na damu ya Yesu ili asamehewe, hupatanishwa na Mungu (HUWA NA AMANI NA MUNGU SI UADUI), pia hatia ya dhambi huondolewa moyoni kwa damu ili awe na utulivu kwa Roho Mtakatifu, utulivu huu ni amani.


Usikose sehemu ya Mwisho ya Somo Hili, ambapo Tutaangalia Umuhimu wa Amani katika Maisha Yetu na Funguo za Kuipata Amani. MUNGU Akubariki kwa Kuendelea Kujifunza.

No comments:

Post a Comment