Vita
Vizuri vya Imani
Katika
maandiko, Habakuki 2:4, Inaonyesha mwenye haki ataishi kwa imani. Hii
pia imeonekana agano jipya; Warumi 1 :17, Wagalatia 3 : 11 na
Waebrania 10:38. Maisha ya wenye haki ni imani yao, kwa upande
mwingine kifo chake ni pale imani yake inapokufa.
Hapa
tunagundua siri ambayo ni hii “Shetani
anawinda imani ya wenye haki kuliko kitu kingine chochote”,
kwa nini? Kwa kuwa imani ndiyo inakufanya uishi kama Mungu aishivyo,
imani inakuunganisha na Mungu. Mungu anakuja kwako, na wewe unaenda
kwa Mungu, kiunganishi ni imani. Kwa mfano, Mathayo 19:26-27,
inasema, yote yanawezekana kwa Mungu. Marko 9:23, inasema yote
yanawezekana kwake aaminiye. Hivyo ni kusema mtu anakuwa kama Mungu
alivyo katika utendaji wake, ikiwepo imani; bila shaka Shetani
anachukia imani kwa sababu hii. Hatimaye huja kuipinga au kujaribu
kuidhoofisha. Katika sehemu ya kwanza tumeangalia imani kwa ujumla
na mambo yapaswayo kufanya ili kuichochea. Sehemu hii ya pili ni ya
vita ambayo hufanywa kwa kulinda imani au kuishindania na kwa njia
ya kuitumia kumpinga Shetani kwa ahadi za Mungu.
Biblia
Inasema
Mpingeni
huyo mkiwa thabiti katika imani (1 Petro 5:9). Kwa kuwa andiko hili
limesema hivi, Shetani hafurahii imani, maana kuwepo kwa imani
zetu ni kupingwa kwake. Imani haimleti Mungu duniani tu! Bali
inampinga Shetani, inamzuia kutenda kazi, inamwondoa duniani, si
kwamba inamfanya asiwepo duniani, bali inamzuia, inamdhibiti.
Yuda
aliandika, “Mwishindanie
imani waliokabidhiwa watakatifu mara moja tu”(Yuda
1:3). Neno la Kiyunani lililotumika kuonnyesha kuishindania imani
katika andiko hili ni “epagonizomai”,
maana yake ni kushindana kinyume na wengine, ni kushindana na
mafundisho ya uongo waliyofundisha wengine, yaliyokuwa kinyume na Injili ya Kristo au imani ya Kristo.
Hapa
utagundua pia, Shetani anaharibu imani ya wokovu kwa kuleta
mafundisho ya uongo.
Silaha
Atumiazo
Silaha
anazotumia kupinga imani ni 1. Mawazo ya uongo 2. Mazingira hasi 3.
Maneno ya watu 4. Hisia za uongo 5. Mafundisho ya uongo 6. Muda,
kuchelewesha kutimia kwa ahadi kwa kutumia nguvu za giza 7. Mwenendo
usio sahihi, kuchochea matendo ya mwili. Vita vizuri vya imani
tunavipiga maeneo hayo yote.
Imani
inakaa moyoni na inao uhusiano na Mungu moja kwa moja. Shetani
akitaka kuishambulia na kuiua anatumia mashaka.
Mashaka ni kutokuwa na msimamo mmoja, kuwa pande mbili wakati mmoja.
Njia ya kuleta mashaka ni kuuliza maswali kuhusu udhahiri au
bayana ya Mungu na neno lake. Maswali haya kwa sehemu kubwa anayaleta
katika mawazo.
Anaweza
kutumia mazingira ya muda na kuuliza “mbona
siku zinaenda
na
sioni matokeo? labda Mungu hajasikia”
mawazo haya ya kujiuliza kuhusu Mungu au Neno lake huleta mashaka.
Hapa Shetani hushambulia uhakika ili kuua uhakika, kwa kuleta
wasiwasi katika udhahiri wako wa ndani, yaani Mungu na Neno lake.
Kama
wewe ni binti hujaolewa na umemwamini Mungu, kwa kuwa imeandikwa mtu
atamwacha baba na mama yake na kuambatana na mke wake. Jaribu la
kwanza unaloweza kupata, Shetani atatumia muda kusema nawe katika
mawazo. Utapata mawazo yasemayo “muda
unaenda sasa
nina
miaka 33, ikifika miaka 40 kuna hatari nikashindwa kuzaa hata
nikiolewa
…….” Haya si mawazo yako tu ni mashaka yanayopandwa na Shetani,
hupiga matumaini ili kuua imani. Anajaribu kuiua kwa kupiga matumaini
na udhahiri wa ndani.
Mara
nyingine, wakati mawazo hayo yanakujia anaweza kutokea mtu wa karibu
na kusema, “Hee!unazidi
kuzeeka tu! Utaolewa lini?”
Hapa adui anamtumia mtu kuuwa matumaini. Mara nyingine baada tu ya
mtu kumpa Yesu maisha yake, na kuwa na uhakika wa dhahiri ndani yake
kuwa ameokoka. Mazingira ya nje hubadilika kabisa. Ataanza kupata
mateso na kukataliwa. Baada ya hapo atakosa matumaini na mawazo kama
haya yanamjia “afadhali
nilivyokuwa sijaokoka”.
Hapa Shetani anapiga tumaini lako ili kuua uhalisi wako wa ndani kuwa
umeokoka. Mara nyingine wazo kama hili huja “Mungu
si mkweli anasema nikimwamini Yesu nitaokoka, mbona sasa matatizo
tu!”
Hapa Shetani anapinga udhahiri wa Mungu na Neno lake kuua uhakika wa
moyoni, kwa kumshitaki Mungu katika nafsi yako.
Akishindwa
kukuangusha kwa kutumia dhiki, atatafuta kukuangusha imani yako kwa
mafundisho ya uongo, ya kukupotosha. Kanisa la kwanza lilipata dhiki,
baadaye ukaja upotefu wa imani.
Mbali
na mawazo, njia nyingine atumiayo adui ni hisia. Hisia hapa nina
maana ya; kuona, kugusa, kusikia, kunusa na kuonja. Unaweza kuomba
jambo na kuliona moyoni kuwa na uhakika umelipokea kwa udhahiri wa
Neno la Mungu. Vita itakayototea ni hii “Kiko
wapi nilichoomba? mbona sijisikii ninacho?”.
Hapa jambo la kufanya ni kuamini kwa njia ya kusema Neno linasemaje,
na kutafakari unavyoona uhakika wa ndani. Baadaye hisia
zitabadilika.
Jinsi
mwenendo wetu ulivyo, au jinsi tunavyoishi haiwezi kutenganishwa na
imani zetu. Jinsi Imani ilivyo kwa Yesu ndivyo jinsi tutakavyoenenda
kitabia, tabia unayoishi sasa inaonyesha utakuwaje milele. Maandiko
yanasemaje, “lakini
mwenendo wenu na uwe kama inavyoipasa injili ya Kristo
…….” ( Wafilipi 1 : 27). Ndani ya injili kuna imani, “kwa
maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake toka imani hata
imani..……
“(Warumi 1 : 17). Kwa hiyo Paulo angeweza kusema “lakini
mwenendo wenu na uwe kama inavyoipasa Imani ya Kristo”
au “mwenendo
wenu uwe kama yanavyopasa
maisha
ya Kristo”.
Kuishi injili ya Kristo ni kuishi imani ya Kristo. Haya ni maisha ya
Kristo. Shetani hushambulia eneo hilo la mwenendo wa Kristo katika
maisha yetu. Kwa nini anafanya hivyo? Anajua jinsi unavyoenenda
sasa,matendo tuendayo yanaambatana na sisi milele (Ufunuo 14:13).
Mwenendo wa imani ya wokovu ni matendo ya upendo. Shetani atapinga
tusiendende kwa Roho yaani Upendo ili imani zetu zisiwe na matunda.
No comments:
Post a Comment