Jinsi
ya Kupigana Vita viziri vya Imani
Paulo
alimwandikia Timotheo maandiko haya “Mwanangu
Timotheo nakukabidhi agizo hilo liwe akiba, kwa ajili ya maneno ya
unabii yaliyotangulia juu yako, ili katika hayo uvipige vile vita
vizuri”
(1 Timotheo 1:18). Vita hivi vizuri vinavyotajwa na andiko hili ni
vipi? Andiko lifuatalo linatoa jibu, “Piga
vita vile vizuri vya imani, ……..
“( 1Timotheo 6:12). Kwa nini vita hivi vinapigwa? Vinapigwa ili
kuilinda
imani mpaka matarajio yatokee, anasema tena Paulo “nimevipiga
vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, imani nimeilinda.”
(2Timoteo 4:7). Baada ya kuilinda imani matarajio yake au matumaini
yanaenda kudhihirika “ baada
ya hayo nimewekewa taji ya haki ………….. “
(2Timoteo 4:8). Maandiko hayo yote yanatufundisha mambo yafuatayo:-
1.
Vita vizuri vinapigwa kwa kutumia maneno ya unabii ( Neno la Mungu)
2.
Vita hivi vizuri ni vita vya imani
3.Vita
hivi vinapigwa kuilinda imani mpaka itakapo dhihirishwa madhihirisho
yote, yanayotarajiwa.
Kipele
Kilichokuwa Usoni
Wakati
fulani nilikuwa na kiupele cha kuzaliwa nacho usoni na kilinikosesha
raha. Ilifikia wakati nikakiamuru kiondoke kwa jina la Yesu. Niliona
moyoni, Yohana 14:13 ni dhahiri na nikawa na uhakika (pistis), kwamba
nikisema tu kitaondoka. Nilisema kwa jina la Yesu kiondoke na moyoni
nikaona kimeondoka. Ingawa kilikuwepo nje moyoni hakikuwepo tena!
Baada ya hapo nikaendelea kuamini (pisteuo) kwa njia ya shukrani,
kutafakari Yohana 14:13, sifa, pia kuamuru udhihirisho utoke nje
ambao tayari ninao moyoni. Matarajio yangu ya kuona udhihirisho ya
kawa hai wakati wote. Nikijiona katika kioo nilikuwa naona kipele,
Shetani alisema mawazoni “bado
kipo”
na mimi nikapiga vita vya imani kwa kuamini na kusema toka moyoni
“Kimeondoka……”
vita vya imani vinapiganiwa katika moyo na mawazo au mazingira kwa
kutumia Neno la unabii, maandiko na jina la Yesu.
Mungu
hujenga udhahiri wa Neno
moyoni,
Shetani hujenge maswali na mashaka akilini. Baadaye kipele kile
kilipotea usoni, ingawa kilipotea siku nyingi moyoni. Niliyapata
niliyotarajia kwa kuvumilia na kupiga vita kwa kuamini, Kwa kutenda
mambo kinyume na mazingira.
Goita
Ilipotea
Mtumishi
wa Mungu Smith Wigglesworth alitoa ushuhuda wa mwanamke mmoja
aliyeombewa katika mkutano wake, akiwa na ugonjwa wa goita. Baada ya kuombewa moyoni alipata uhakika goita imetoka. Aliona ni
halisi imetoka kama Mungu alivyosema katika Neno. Alikuwa
akijiangalia kwenye kioo na kusema goita haipo (haikuwepo moyoni
katika Imani) ingawa ilikuwa inaonekana. Ilipita miaka takribani
mitatu akiendelea kusema hivyo. Siku moja alishuhudia katika mkutano
kwamba goita imetoka, watu walimcheka! Mmoja akamwita pembeni na
kumwambia aache kusema hivyo anakuwa kama kichaa, wamesikia vya
kutosha. Muda si mrefu ikapotea! Watu walipomuuliza akawajibu
ilishapotea miaka mitatu iliyopita! Vita vya imani alivyopigana
mwanamke huyu, vilihusiana na maneno ya watu, muda na mazingira
ya ugonjwa kuwepo, alitarajia yasiyoweza kutarajiwa si kwa imani tu,
bali pia kwa kuamini.
Mitume
Wakati wa Kanisa la Kwanza
Wakati
mitume wanahuburi injili, mara kwa mara walikutana na
upinzani. Hasa kutoka kwa viongozi wa dini. Waliwakataza wasihubiri
kwa jina la Yesu (Matendo 4: 16-19). Hii ilikuwa ni imani ya Yesu
inapingwa. Vita vizuri vya Imani vilipigwa kwa kusema yafuatayo kwa wapinzani, “…..
maana hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia”
(Matendo 4:20).
Mitume
walishindania imani kwa kufanya atakavyo Mungu aliyekuwa dhahiri
ndani yao, na kutii agizo ambalo Yesu aliwaagiza kuhubiri injili kwa
kila kiumbe bila shaka lilikuwa dhahiri kwao. Hatimaye wakawa na
uhakika mkuu wa walichofanya. Hii ilikuwa ni imani iliyoweza mpinga
Shetani na matakwa yake ya kuzuia kuhubiriwa injili, alitaka kuzuia
kupitia watu viongozi wa dini.
Kwa
kanisa la Pergamo (Ufunuo 2:12-13), Yesu alisema, likaapo kanisa hilo
ndipo penye sinagogi la Shetani. Lakini akalisifu kwamba halikuikana
imani ya Yesu kwasababu ya dhiki za kishetani! Hili ni kanisa ambalo
lilikuwa tayari kuifia imani. Mtu aliyeokoka kweli, lazima awe
mwanafunzi wa Yesu. Mtu aliye tayari kufa kwa ajili ya imani ya Yesu
ni mwanafunzi wa Yesu.
No comments:
Post a Comment