Mtu awashapo moto,
mfano awashapo jiko la mkaa ili uweke kwa haraka inampasa auchochee kwa kuupuliza.
Vichocheo
vya Imani
Kama
vile moto huchechewa kwa upepo, Imani huchochewa kwa kufahamu moyoni.
Kufahamu moyoni ya kwamba Mungu ni bayana na neno lake alilosema
ni bayana. Hii huleta uhakika wa sasa kwamba kile alichosema anatenda hata kama
sio dhahiri, yaani hata kama hatuoni akitenda. Lakini ni dhahiri anatenda na yupo
ingawa hatumuoni, kama mawimbi ya redio
yalivyo dhahiri na sauti za watu na
nyimbo ingawa hatuyaoni!
Uhakika wa mambo tutarajiayo
ambayo sasa tunayo kwa Mungu na Neno lake unachochewa
na ufahamu atupao Roho Mtakatifu. Kuhusu
Mungu na Neno lake. Imani hushika mambo yajayo sasa, katika Mungu na Neno lake moyoni.
Vichocheo
vya Tumaini
Tumaini ni matarajio
ya akilini kwamba mambo tuliopokea moyoni kwa imani yanaenda kudhihilika
au kuonekana. Tumaini limefungwa na muda wa udhihirisho, imani haina muda, yote
yameshatimia sasa kwa imani, Kama alivyo Mungu
ni wa milele yote yametimia kwake. Tumaini huyangojea kwa wakati na majira
yadhihirike. Tumaini limefungwa na muda. Kichocheo cha tumaini ni kuamini( pisteuo), ni kuitenda imani ya
moyoni. Ili
tumaini lisife lazima kuifanyia kazi imani au kuitenda imani.
Imani inabeba tumaini au matarajio matumaini huzalishwa
kwa kuamini, kusema neno, kutenda, kushukuru
huku ni kuitendea kazi imani.
Angalia
Mifano Hii
Maandiko yanasema “Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno
la kweli, habari njema za wokovu wenu:tena mmekwisha kumwamini yeye na kutiwa
muhuri na Roho Yule wa ahadi aliye Mtakatifu
ndiye aliye arabuni ya urithi wetu
ili kuleta ukombozi wa milki yake,” (Waefeso 1: 13-14).
Katika andiko hili Roho wa Mungu anaonekana katika
maisha yetu kama Muhuri na Arabuni. Mambo
haya mawili yanachochea imani natumaini letu katika Kristo Yesu.
Muhuri
Katika Ufunuo 20:3,
inaonyesha malaika alipomtia Shetani katika shimo la kuzimu, aliweka muhuri
baada ya kulifunga, ili asipate kuwadanganya Mataifa tena. Kwa maneno mengine
muhuri ulileta usalama, Mataifa
wasidanganywe.
Katika Yohana 6:27, Maandiko
yanasema, Yesu ametiwa muhuri na Baba. Tafsiri rahisi ni kwamba Yesu amethibitishwa na Baba. Muhuri
huthibitisha.
Katika Waefeso 4:30,
Roho Mtakatifu anaonekana kama Muhuri wa kuhifadhi. Maandiko haya yanasema kwa
yeye tumetiwa muhuri hata siku ya ukombozi. Tumetengwa na muhuri huo hata
ukombozi wa miili yetu utakapotokea. Pia muhuri ni ishara ya umiliki. Watakaotiwa muhuri katika ufunuo 7:3-8, itakuwa
ni ishara ya kwamba watamilikiwa na Mungu.
Kwa hiyo Roho Mtakatifu kama Muhuri katika maisha
yetu ni ishara kwamba tupo salama milele, tumethibitishwa, tumehifadhiwa, tunamilikuwa
na Mungu. Amefanyika Muhuri tulipozaliwa na yeye au tulipofanywa wana wa Mungu
(Warumi 8: 15, Yohana 3:6).
Kwa kufahamu Roho ni
Muhuri, inachochea uhalisi wa wokovu ndani yetu sasa, hii ni imani ya
wokovu. Pia inachochea matarajio ya
kuingia Mbinguni, wakati ujao hili ni tumaini letu. Ikiwa utasema, utamshukuru
Mungu na kuwaza haya, yaani Roho ni Muhuri wako, imani yako na umaini la wokovu
litakuwa imara.
Arabuni
Arabuni maana yake ni
malipo ya kwanza “deposit” (2 Wakorintho
1:22, 5:5). Tulipofanywa wana baadaya kumwamini Yesu, Roho Mtakatifu alifanyika
malipo ya kwanza na ukombozi wetu wa milele. Bado hatujamwona Baba, bado
hujaona mbinguni, bado hatujaona urithi wetu wote ulio mkubwa mbinguni. Pamoja
na hayo Mungu ametuonyesha kwa kutupa Arabuni ya Roho. Huyu ni kama kishika uchumba anaethibitisha siku moja, ndoa
itafanyika na Yesu mbinguni. Yeye ni
uthibisho kwamba sisi ni mali
ya Mungu ameshatulupia sehemu ya kwanza.
Sehemu ya pili tutaipata katika umilele mbinguni, ya kwanza ni Arabuni
ya Roho duniani.
Ni sawa na mtu
alieenda dukani kununua kiatu cha elfu hamsini. Anaweza kutoa elfu ishirini kama arabuni na baadaye akalipa elfu thelathini. Elfu
ishirini aliyotoa itathibitisha kiatu kile ni mali yake na majira timilifu yakija
atakichukua. Ndivyo alivyofanya Baba. Ametupa Roho kuonyesha sisi ni milki yake
ni mali
yake, siku moja atatumiliki milele mbinguni.
Kufahamu ukweli huu inachochea
uhalisi au uhakika wa wokovu wetu sasa. Pia inajenga matumaini makuu ya kuishi
na Mungu, wakati ujao. Tunaposema, tunaposhukuru, tunapotafakari au tunapotendea
kazi Imani yetu matunaini ya udhihilisho wa kuingia Mbinguni yanakuwa hai na tunampendeza Mungu tunajitakasa
kwa kuwa sisi si wa dunia hii
(1Yohana3:1-3). Tumaini la wokovu wa
milele likiwepo, utakatifu huja. Pasipokuwa na matumaini watu hutenda dhambi,
maana hakuna wanachotarajia mbele. Kwa hiyo katika vita vya kiroho Shetani
hupiga matumaini vita, ili watu wasiwe watakatifu. Maandiko yanasema “Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihilika bado
tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihilishwa, tutafanana naye; kwa
maana tutamwona kama alivyo. Na kila mwenye matumaini
haya katika yeye hujitakasa kama yeye alivyo
mtakatifu. “(1 Yohana 3 : 2-3). Huwezi
kujitakasa usipojua tumaini lako. Tumaini haliwi hai usipoamini. Pia huwezi
kuamini bila imani au uhalisi wa ndani. Hamna uhalisi wa moyoni bila udhahiri bayana wa Mungu na Neno lake. Kumfahamu Roho
kama Arabuni kwa Neno la Mungu, inachochea Imani, kuamini, matumaini na
utakatifu.
No comments:
Post a Comment