Ifahamu Imani na Upendo
Ili kuweza kuishi
kwa imani itendayo kazi ni lazima ufahamu ya kuwa imani yako hufanya kazi
pamoja na upendo. Kama
vile samaki asivyoweza kuishi akitolewa nje ya maji, imani haiwezi kuishi au
kutoa matunda yadumuyo isipokuwa ndani ya upendo. Msingi wa imani ya kweli mbele za Mungu ni
upendo. Maandiko yanasema, “Maana katika Kristo Yesu kutairiwa hakufai
neno, wala kutotahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo” (Wagalatia
5:6).
Kuishi kwa Upendo ni nini?
Kwa kuwa tumefahamu
kwamba imani inatenda kazi kwa msingi wa upendo, ni muhimu tuelewe tunaishije
kwa upendo.
Kuzishika/ Kuzitii Amri za Mungu
Maandiko yanasema, “Kutahiriwa si kitu, na kutokutahiriwa si kitu bali kuzihifadhi amri za Mungu” (1 Wakorintho 7:19). Kuzihifadhi amri au kuzishika amri ni
kumpenda Mungu, ni kuishi kwa upendo mbele za Mungu. Yesu alisema, “Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye;…”
(Yohana 14:21). Mtumishi wa Mungu Yohana
kwa Roho Mtakatifu aliandika, “Kwa maana
huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike
amri zake; wala amri zake si nzito.” (1Yohana 5:3). Maandiko haya yote yanaonyesha ya kuwa
kumpenda Mungu ni kuzishika amri zake.
Unazishika amri zake ingawa hatumuoni.
Ndani yetu una uhakika yeye ni dhahiri ni bayana ndio maana tuna mtii.
Tunapoishi
kwa kumtii Mungu, yaani tunapoishi kwa kulitii Neno lake ni
udhihirisho kuwa tunampenda. Ikiwa
unampenda mtu si rahisi kuacha kufanya anachokuambia. Tumpendapo Mungu
tutafanya ayatakayo. Ingawa hatumwoni
kwa macho, mioyo yetu inamwona dhahiri yupo kwa njia ya Neno lake. Katika hali
ya kumpenda ni rahisi kuwa na ujasiri mbele zake maana dhamiri zetu hazita
tushitaki kwa kosa lolote.[1] Ujasiri huu utatuwezesha kuomba kwa imani na
kupokea. Kwa maneno mengine imani yako katika maombi itafanya kazi
kwa kuwa umempenda Mungu kwa kumtii
hata kuwa na ujasiri mbele zake.
Maandiko yanasema, “ na lolote
tuombalo (Tuombalo kwa imani), twalipokea
kwake, kwa kuwa twazishika amri zake(twampenda twaenenda kwa upendo), na kuyatenda yapendezayo machoni pake.”
(1 Yohana 3:22).
1.
Kuishi kwa Mwongozo wa Roho Mtakatifu/ Kuishi kama Viumbe Vipya
Tunapookoka/tunapompa
Yesu maisha yetu tunafanyika viumbe vipya.
Katika utu wa ndani tunakuwa tumezaliwa na Mungu, hivyo tunafanana na
Mungu aliye Upendo. Kila mtu aliyempokea
Yesu/ aliyezaliwa mara ya pili, anao upendo wa Mungu ndani yake (Warumi 5:5). Inawezekana hautumii au haishi kwa kuongozwa
na upendo, lakini tayari umepandwa ndani kwa njia ya Roho Mtakatifu. Maandiko yanasema, “Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya
(au kuzaliwa mara ya pili)” (Wagalatia 6:15).
Kuzaliwa mara ya pili kumefanyika kwa njia ya Mungu Roho Mtakatifu ndani
yetu, “Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili;
na kilichozaliwa kwa Roho ni roho” (Yohana 3:6). Ikiwa mtu amezaliwa kwa Roho Mtakatifu kwa
njia ya kumwamini Yesu, katika upya huo wa kiroho, Roho wa Mungu huanza
kumuongoza mtu huyo kwa njia ya tunda la Roho, yaani upendo. Roho
Mtakatifu anamsaidia mtu huyo kupenda, kupenda ni; kusamehe, kuvumilia, kufadhili, kutohesabu mabaya, kuwa na
amani, kuwa na furaha, nk. Maisha ya namna hii ni maisha ya upendo yaiwezeshayo imani ya mtu
aliyeokoka kufanya kazi.
Maneno Aliyosema Yesu
Mifano ya utendaji wa
imani pamoja na upendo tunaweza kuipata katika mafundisho aliyofundisha
Yesu. Alisema, “Nanyi msimamapo na kusali (kusali
ni tendo la imani), sameheni (kusamehe ni tendo la upendo), mkiwa na neno juu ya mtu;…”(Mathayo 11:25). Mahali pengine alisema, “Basi ukileta sadaka yako (kitendo cha kutoa/kuleta sadaka ni
kitendo cha imani) madhabahuni na huku
ukikumbuka ndugu yako ana neno juu yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu,
uende zako, upatane kwanza na ndugu yako(kupatana
na ndugu ni upendo), kisha urudi uitoe
sadaka yako.” (Mathayo 5:24-25). Kwa
maandiko haya tunagundua kuwa huwezi kuchukuwa hatua ya imani ya kuomba au
kutoa, ikiwa una tatizo katika upendo, yaani haujasamehe au haujamtii Mungu.
Upendo ndani yako unajenga uhalisi na ujasiri wa kupokea mambo unayoarajia.
Ili
kuchochea utendaji wa imani yako ni lazima utafute sana kuishi kwa upendo mbele za Mungu na
watu. Ukiishi kwa upendo utafahamu kuwa
Mungu yuko upande wako na anaiheshimu imani yako. Utakuwa na ujasiri mbele zake kwa kuwa hauna
hatia kwake, umemtii, unampenda. Ufahamu
huu utaichochea imani, uhalisi wa ndani, kutegemea muujiza toka kwa Mungu wako.
Chochea
imani yako kwa njia ya kumtii Mungu na maneno yake yote, na kuwa na amani na
watu wote. Kisha utakuwa na ujasiri wa
kupokea kwa imani toka kwa Mung
No comments:
Post a Comment