Utangulizi
Imani
ni nini? Maandiko yanasema “Imani ni kuwa
na hakika ya mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasioonekana” (Waebrania
11:1). Andiko hili linaonyesha imani ikitafsiriwa meoneo mawili: 1. Kuwa na
uhakika wa mambo yatalajiwayo 2. Bayana
ya mambo yasioonekana.
Kuwa na Hakika.
Kipengele
hiki cha kuwa na hakika kinahusiana na moyo. Ni kuwa na uhakika moyoni. Tafsili halisi ya kuwa na
uhakika ni “ kuwa na uhalisi”. Neno
la Kiyunani linalotumika kuonyosha uhakika katika andiko hili ni “hupostasis”, ambalo linaonyesha kitu
halisi ambacho kitu kingine kinajengwa juu yake, kwa mfano msingi wa nyumba ni
kitu halisi ambacho myumba inajangwa juu yake. Kwa namna hiyo hiyo, imani ni
msingi ni uhalisi wa moyoni wa mambo
unayotarajia kutokea wazi, Yadhihirike mwilini. Imani ni uhalisi wa sasa
ndani yako wa mambo unayotarajia kuyaona
nje baadaye. Imani inapokea sasa
kitu ambacho hakijaonekana.
Tafsiri hii inatoka
katika neon la Kiyunani “pistis”, Neno
hili ni jina. Tendo lake linaitwa “pisteuo”
yaani kuamini, kuamini ni kuitendea kazi imani iliyopekea sasa,
mambo yatarajiwayo kuokea au kudhihirika. Imani ya moyoni hudhihirisha
yaarajiwayo kutokea kwa njia ya kuamini; Kwa mfano kuomba, kushukuru, kutenda
jambo lililosemwa na ahadi nk. Imani inadhihirishwa kwa kuamini, kuamini kunadhihirisha
yaarajiwayo.Kabla hujaona jambo unalotarajia linatokea, lazima msingi wa jambo
hilo ujengwe, unaitwa uhakika ua uhalisi wa jambo hilo sasa katika moyo.
Bayana ya Yasioonekana
Imani pia inafanya
kazi na mambo bayana au dhahiri yasioonekana.
Mambo hayo ni: Mungu na Neno lake.
Mungu na Neno ni dhahiri ingawa hawaonekani; ni kama vile upepo upo
dhahiri / bayana lakina hauonekani. Neno
la Mungu pia ni dhahiri ingawa halionekani, ni kama vile mawimbi ya redio, yalivyo bayana
ingawa hayaonekani. Uhalisi wa ndani sasa
hujengwa na udhahiri usioonekana, yaani Mungu na Neno lake. Moyo uonapo
udhahiri wa Mungu na Neno lake, kwamba yale aliyosema ni kweli na yanatimia,
hujenga uhalisi /uhakika. Uhakika huu hubeba matarajio ya kuona jambo likitimia mwilini. Kwa lugha
rahisi tunaweza kusema, matarajio ya jambo kutokea kujengwa, Hujeengwa juu ya
uhakika wa sasa moyoni, uhakika huu hujengwa na ubayana wa Mungu na Neno lake. Shetani anatafuta imani aiuwe kwa hiyo
yatupasa tuishindanie au tuilinde. Kulinda imani ni kupigana vita vizuri vya
imani. Kwa upande mwingine Mungu huitumia imani yetu tushirikiane naye na
kumpingani Shetani. Kumpinga Shetani kwa imani kwa njia ya ahadi za Mungu ni
vita vya imani.
Kwa upande mwingine Mungu
tunampendeza kwa imani. Ukitaka kufanya mapenzi ya Mungu kitu cha kwanza
kukitafuta na kukielewa ni imani. Maandiko yanasema pasipo imani haiwezekani
kumpendeza (Waebrania 11:6). Maandiko mengine
yanasema, “Angalieni, ndugu zangu, usiwe
katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hai.”
(Waebrania 3:12). Andiko hili linaonyesha kwamba kuwa na moyo mbovu ni
kutokuamini, moyo wa namna hii ni moyo uliojitenga na Mungu! Msitari wa 19 unasema, “Basi twaona ya kuwa hawakuweza kuingia kwasababu ya kutokuamini kwao”. Hawakuingia
kwa kuasi, Kutokuamini ni kama kumwasi
Mungu, watu hawa hawakuingia Kaanani kwa kutoamini, kuasi, “ Tena ni kina nani aliowaapia ya kwamba
hawataingia katika raha yake, ila si wale walioasi?”(Waebrania 3:19). Yesu
alionyesha kutokuamini ni dhambi, “Kwa
habari ya dhambi, kwasababu hawaniamini mini;…”( Yohana 16:9).
Kutokumwamini Yesu ni dhambi na ni chanzo cha dhambi zote. Kwa hiyo ni vema
kuielewa imani ili kuweza kumpendeza Mungu, kuishi naye, kutokumwasi na kuingia
katika ahadi zetu tulizopewa, ikiwemo ya kuingia mbinguni.
Kitabu hiki
ni toleo la pili. Toleo la kwanza liliitwa Chochea Imani Yako. Katika toleo
hili kuna mambo mengi mapya ni vyema
kama ulishakisoma, kusoma upya.
No comments:
Post a Comment