Saturday, August 2, 2014

Usimchukie Mungu

Kumchukia Mungu

INAWEZEKANA UNAJUA MAANA YA KUMPENDA MUNGU, LAKINI HUJUI KUMCHUKIA MUNGU NI NINI. KATIKA SOMO HILI UTAJIFUNZA MAANA YA KUMCHIKIA MUNGU. KISHA JILINDE USIMCHUKIE.
                     Warumi 1:28-30
Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa , wayafanye yasiyowapasa. Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda na uuwaji, na fitina na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya. Wenye kusingizia , wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao.
      KUMCHUKIA MUNGU NI NINI?
1. Kumchukia Mtu Aliyebadilishwa na Neno (Yohana 17:14-16)
Mtu aliyeokoka
Mtu anayesema ukweli katika Yesu
Kumchukia mtumishi wa kweli wa Mungu.
Usikwazwe na mtu wa Mungu, ikiwa anaomba sana au jambo lingine la Mungu. Utatenda tendo la kumchukia Mungu.
2. Kupenda Dunia (1Yohana 2:16-17)
Kupenda dunia ni kudhibitiwa na mfumo uliopo duniani usio na Mungu ndani yake.  Mfumo huu huchochea uovu na tamaa.
Dunia ni mfumo unaomvuta mtu kwenye tamaa na dhambi, ingawa wenyewe sio dhambi. Kwa mfano disco ni roho ya dunia, ukienda kuna tamaa ya uzinzi, nk.
3. Kukasirika baada ya kuonywa na Mungu (Yohana 7:7).
Kutotaka kuonywa na Mungu baada ya kumkosea ni dalili ya kumchukia.
Kutotaka Neno liweze kumwonya mtu ni dalili ya kumchukia Mungu.
Mungu akikuonya kwa Neno kubali kwa kunyenyekea. Usipofanya hivyo ni dalili ya kumckukia.

                      USIMCHUKIE MUNGU

No comments:

Post a Comment