Nguvu ya Jina la Yesu
Jina la Yesu tumepewa sio kwaajili
ya kuombea wagonjwa na kutoa pepo tu.
Tumepewa jina hili tulitumie katika mazingira yote tuliyo nayo. Maandiko yanasema, “Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la
Bwana Yesu,…” (Wakolosai 3:17).
Katika huduma na maisha yake, mama Mbise ameonekana kulitumia jina la
Yesu si katika maombi kwa wenye shida tu, bali hata katika maisha ya kila
siku. Kama
anavyoshuhudia katika maneno haya:
Miaka ya tisini nilikwenda eneo la Sakila katika huduma
ya ushuhuda wa nyumba kwa nyumba.
Tukaingia katika nyumba ya mzee mmoja aitwaye Mathayo. Alikuwa na ugonjwa wa pumu ambao
ulisababishwa na pepo. Wakati tunamwombea
pepo alitamka na kusema haondoki. Karibu
na mlango kulikuwa na mbwa wake. Yule
baba alikuwa amelala chini anaangalia wale mbwa wakati tunaendelea kuomba. Mara
nyingine tena nikamwamuru yule pepo na kusema, “kwa jina la Yesu toka”. Mara mbwa mmoja pale nje akakohoa kama
aliyebanwa na pumu akajinyoosha na kufa.
Ghafla yule baba akainuka na kusema amefunguka. Baba huyu aliogopa sana akasema, “jamani
naomba mniombee maana kuna Mungu” (Hii ilikuwa ni ishara iliyomfungua
macho mgonjwa huyu, akatambua kwamba kuna Mungu mara tu alipopona. Uponyaji huu
ulikuwa ishara kwake, ishara mara nyingi ni uponyaji, muujiza au ufunuo ambao
unaashiria kwamba Mungu yupo nyuma ya utendaji huo na kumvuta mtu kumwamini au
kumtukuza.) Yesu alipofanya muujiza wa
kugeuza maji kuwa divai (Yohana 2:1-11), muujiza huu ulikuwa ni ishara au
ufunguo kwa wanafunzi, maana walifumbuliwa macho na wakamwamini. Mtumishi anaendelea kushuhudia kwa kusema:
Kwa kumfungua mzee huyu kutoka kwenye pumu Mungu
alionyesha kwamba uhai wa mtu una thamani kuliko mnyama. Ndio maana aliruhusu mbwa yule afe kwa
kuingiliwa na pepo aliyetoka ndani ya mtu na mtu akapona.
No comments:
Post a Comment