Ibrahim na Mungu
Katika kitabu cha Mwanzo mlango
wa 15 tunaona Mungu akifanya Agano na Ibrahimu kwa kumwambia ampatie wanyama
kisha akapita katikati yao
kwa mwenge wa moto. Alilithibitisha Agano yeye mwenyewe. Katika Agano Jipya
Yesu alifanya Agano na wanadamu kwa njia ya kuutoa mwili wake na kumwaga damu
yake na kila amwaminiye kama ni Myahudi au
Mmataifa huiingia katika Agano.
Sura ya Kristo kwa Ibrahimu
ilitokea kwa mfano wa kuhani Melkizedeki aliyeitwa kuhani wa Mungu aliye juu sana na mfalme wa
Salemu(Mwanzo 14:17-20). Huyu alileta mkate
na divai kwa Ibrahimu. Mkate tunaweza kuufananisha na mwili wa Yesu katika
Agano Jipya na divai ni damu yake. Melkizedeki amefananishwa na Kristo katika
Agano Jipya (Waebrania 7:1,2, 10-22). Ibrahimu alimpa Melkizedeki sehemu ya
kumi ya vitu vyote alivyokuwa navyo. Katika Agano Jipya Yesu aliyekuja kwa
mwili na damu yake kufanya Agano nasi, tunatoa sehemu ya kumi kwake, kama Ibrahimu alivyotoa kwa Melkizedeki. Kitendo cha
kutoa sehemu ya kumi ni kitendo cha kiagano kwa yule aliyefanya Agano nasi
yaani Yesu. Kwa hiyo kama Ibrahimu alikuwa baba yetu wa Imani naye alitoa
sehemu ya kumi kwa Melkizedeki ambaye ni picha ya ‘Yesu Kristo’ katika Agano la
kale, sisi pia tunaweza kutoa kwake Yesu leo, Sehemu ya kumi katika Agano
Jipya.
No comments:
Post a Comment