Friday, August 8, 2014

KUMWAMINI NA KUMTII



 MWOKOZI NA BWANA


Apeitheo


“Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.”


(Yohana 3:36)


Neno kutomwamini Mwana hapa kwa Kiyunani ni “Apeitheo”.  Mara nyingi ukishuhudia mtu na kumweleza kuhusu Yesu karibu watu wote husema wanamwamini Yesu. Wanaamini yupo na anawapenda nk.
Neno hili asiyemwamini lina maana ya asiyekubaliana na yeye, asiyemtii. Kuamini kwa maana ya kumtegemea Yesu kuhesabiwa haki na kuokolewa huambatana na utii. Imani inaendana na utii.


Umwaminipo Yesu kama Mwokozi ni lazima umtii kama Bwana. Wengi wakati wa sasa humpokea Yesu kama Mwokozi wao, ila hawataki aguse maisha yao, wanataka waishi vile vile walivyokuwa! HAPANA! Utahukumiwa usipokubali Yesu akuongoze maisha yako kama Bwana. Wokovu ni kumwamini Yesu na kusarenda kwake, kuwa tayari kupoteza kila kitu kwaajili ya kumtii Yeye.


“Mtumwa akasema , Bwana hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka…” (Luka 14:22). Maneno haya yanayoonekana hapa ni maneno yanayoonyesha Bwana anavyotakiwa kutendewa. Yanatakiwa yale yaliyosemwa naye yafanywe mara moja! Ni mara ngapi tunasikia Yesu amesema tusamehe, lakini hatusamehi, Mara ngapi tumesikia Yesu anasema tuhubiri injili lakini hatufanyi hivyo! Ni mara ngapi tumesikia Yesu akisema tujifunze kwake lakini hatufanyi hivyo. Mara ngapi tumesikia Yesu amesema imetupasa kuomba siku zote lakini hatuombi. Hebu soma Mathayo 5,6,7 na kisha umfanye Yesu awe Bwana wako leo kwa njia ya  kutii aliyosema hapo.
Wazo Kuu
KUOKOKA NI KUMWAMINI YESU NA KUMTII YESU, HUWEZI KUSHIKA MOJA UKAACHA LINGINE. HUWEZI KUOKOKA NA KUISHI UNAVYOTAKA WEWE, NI ANAVYOTAKA YEYE KWA KUWA NI BWANA WAKO.

No comments:

Post a Comment