Exaleipho
“Akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa kwa
kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena,
akaigongomea msalabani”
(Wakolosai
2:14)
Neno kuifuta hapa tafsiri yake ni kuifuta kabisa pasibaki na
alama yeyote kwamba palikuwa na maandishi.
Sheria ya Musa ilikuwa ni hati halali ya Ki-sheria
iliyotushitaki kwamba sisi ni watenda dhambi na tunastaili mauti.
Kwa hali ya kawaida hatungeweza kutoka katika mashitaka hayo ya
Sheria maana tulikuwa chini ya mwili wenye tamaa ya dhambi. Sheria ikawa na
nguvu ya kutushitaki dhambi kwa kuwa dhambi ilikuwa hai kwa mwili (Warumi 8:3).
Msalabani Yesu alifanya vitu viwili:
1.)Alifuta mashitaka ya
Sheria kwa kifo chake. Alilipia Sheria mauti,
maana ilitaka dhambi zilipiwe mauti. Sasa Sheria imefutwa
mashitaka yake ya kutaka tufe, kwa kuwa kifo cha Yesu kimelipia matakwa hayo
(Warumi 7:1-5).
2.)Amesulubisha mwili wa
dhambi uliyoipa dhambi nguvu ya kufanya kazi ndani ya mtu. Dhambi iliyokaa
mwilini ilimfanya mtu awe adui wa Mungu, maana sheria ilikuwa inaionyesha
wakati wote. Aliposulubiwa alisulubisha
mwili uliotunza dhambi. Kwa njia ya mwili
akafungua njia ya sisi kwenda kwa Mungu. Kwa njia ya damu akatupatanisha na Mungu (Waefeso2:15-16,
Wakolosai 1:20).
Wazo Kuu
Hati ya mashitaka juu yetu iliyotushitaki tufe imefutwa.
Imefutwa kwa kifo cha Yesu. Nguvu yake imeondolewa kwa kuwa ameusulubisha mwili
wa dhambi. Mwili huu uliipa Sheria nguvu ya kuukumu tufe kwa dhambi iliyokuwa
ndani yake. Sasa, Shetani hana pa kutushikia maana alitupata kwa dhambi.
Hatatumia sheria kudai tufe kwa mauti, hatatumia mwili kuchochea tamaa ya
dhambi.
SOMA TENA, OMBA NA KUTAMKA MANENO HAYA KABLA YA KUANZA KAZI
ASUBUHI, PIA KABLA YA KULALA TAFAKARI, AU SHIRIKISHANENI KATIKA KIKUNDI NA
IBADA YA NYUMBANI.
No comments:
Post a Comment