Deigmatizo
“Akiisha
kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya
kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia kwa msalaba huo.”
(Wakolosai
2:15)
Yesu msalabani alipomnyang’anya Shetani mamlaka na kumfanya si
kitu alimfedhehi kwa dhahiri. Alionyesha fedhea ya kushindwa kwake waziwazi.
Neno “Deigmatizo” kwa Kiyunani ni kufedhehesha. Katika Mathayo 1:19, limetumika
kwa maana ya, kuaibisha. Yusufu alikuwa hataki kumwaibisha Mariamu.
Shetani, Wayahudi na Warumi walimwaibisha Yesu msalabani kwa
kumvua nguo, kumtemea mate, kumdhihaki nk.
Kitu cha ajabu msalaba huo huo ukageuka kuwa silaha ya
kumwaibisha Shetani hadharani kwa dhahiri.
Wafalme wa zamani waliposhinda vita, mfalme
aliyeshindwa alifedheheshwa kwa kupitishwa barabarani, kuzomewa, kutupiwa
vinyesi, wakati huo huo aliyeshinda alikuwa akishangiliwa.
Hivi ndivyo ilivyotokea, Yesu alipokufa na kufufuka;
Amemnyanganya Shetani silaha zote, ikiwepo silaha kuu iitwayo mauti! (Ufunuo 1:18).
Amefufuka kwa kushinda, tumshangilie kwa sifa na hapo hapo tutangaze kushindwa
kwa Shetani.Twaweza kufanya hivi katika maombi, sifa au uinjilisti.
WAZO KUU
SIFA, MAOMBI, NA UINJILISTI UAMBATANE NA KUTANGAZA KUSHINDA KWA
YESU NA KUSHINDWA KWA SHETANI. HII ITADHIHIRISHA UKWELI HUO KATIKA MAISHA YETU.
No comments:
Post a Comment