Thursday, June 19, 2014

Uzima Unashinda

Katika kitabu cha Matendo ya Mitume 2:24, inasomeka kwamba, uchungu wa mauti haukuweza kumshika Yesu. Mauti ni uhai wa Shetani. Ni nguvu inayomfanya Shetani awe Shetani. Ufalme wake wote, unaendeshwa na mauti. Pepo wote nguvu yao ni mauti. Mauti makao makuu yake ni kuzimu. Kila mwenye dhambi akifa huenda kuzimu. Mauti humshika na kumzuia kutoka, ina nguvu juu yake kwasababu ya dhambi.

Yesu alipokufa alienda kuzimu. Yeye hakuwa na dhambi, alikufa kwa dhambi zetu. Mauti haikuweza kumshika kuzimu. Mauti haikuwa na nguvu juu yake, kwasababu ni mwenye haki. Mlango wa mauti ni dhambi, mlango wa uzima ni haki ya Yesu. Kwa haki yake akatoka kuzimu kwa nguvu ya ufalme wa Mungu iitwayo, Uzima. Kwa hiyo akashinda mauti. Kwa maana ya nguvu ya ufalme wote wa Shetani.

Ukitubu dhambi leo, ukamwita Yesu aingie ndani yako,atakula na wewe (Ufunuo 3:20). Kula ni kuwa na ushirika. Atashiriki nawe uzima wake. Utakuwa juu ya mauti, yaani nguvu ya Shetani, iliyopo ndani yake na ndani ya mashetani wote! Utawatawala kwa uzima wa Yesu (Warumi 5:17). Kama walivyomshindwa kumshika kuzimu, kwa njia ya uzima wake, hawatakushika wewe duniani, ukiwa kiumbe kipya ndani yake, kwa uzima wake (2 Wakorintho 5:17). Mshiriki Yesu uwe juu ya Shetani, kwa kusema maneno haya:

Sema: Yesu, nakupa maisha yangu. Ingia ndani yangu nami niingie ndani yako. Naacha dhambi zangu kwa haki yako. Kwa haki yako, napokea uzima. Niko juu ya Shetani, dhambi na mauti. Nimeoshwa kwa damu yako. Naamini niliyosema yametokea, huu ni wokovu, AMINA.

2 comments: