Usiutupe Hata Akinguruma
Tunahitaji
ujasiri katika imani zetu ili tupokee
jambo, au tuweze kushindana.
“Basi msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una
thawabu kuu........”
(Waebrania 10:35)
(Waebrania 10:35)
Msitari wa
32 na 33, kabla mwandishi hajawaandikia Waebrania wasiutupe ujasiri, aliandika kwamba
wazikumbuke siku za kwanza baada ya kutiwa nuru walishindana mashindano
makubwa. Waliweza kustahimili mambo magumu na hapohapo kutenda mema. Bila shaka
kitu kilicho wawezesha kuwa hivyo ni ujasiri ndiyo maana msitari huu wa
thelathini na tano akaandika wasiutupe ujasiri
maana uliwasaidia kwanza.
Apobalo
Kutupa
ujasiri ktika andiko hili, ni sawa na kutupa silaha huku ukiogopa! Neno
“Apobalo” la Kiyunani,
lilitumika kuonyesha askari anayetupa silaha huku
akiogopa baada
ya kumwona adui. Kwa lugha nyingine adui huyu alikuwa anafanya vitu vya
kumwogopesha ili autupe ujasiri.
Roho ya woga iletwapo na Shetani shabaha yake ni tutupe ujasiri na kuimbia.
Pasipo ujasiri hatuwezi kusimama na kutumia silaha yeyote!
MAMBO
MUHIMU YA KUYAFAHAMU
1.
Shetani
Hushambulia Ujasiri
(1Petro 5:8)
- Hutishia
kwa kutumia vitu unavyoviona mfano: ukibanwa na kifua au ukiishiwa pesa. Hali
hizi zinaweza kutumika kukufanya uutupe ujasiri katika Bwana. Ukitupa ujasiri huwezi kushindania ushindi wa Yesu.
- Adui
ataweza nguruma kwa hali hizi, kukuonyesha katika
mawazo, ukimwachia
aendelee bila kutamka Neno utatupa
ujasiri na atakupata.
- Hauutupi
ujasiri kwa kumpinga ukiwa thabiti katika imani ya Neno kinywani mwako.
Mfano wa
Daudi Hakutupa
Ujasiri Akatumia Silaha (1Samweli 17:4 – 11)
1.
Shetani alinguruma kupitia
mazingira (Goliati)
2.
Israeli wakatupa ujasiri wao na
kukimbia (17:24)
3.
Daudi hakutupa ujasiri kwasababu hiyo akaweza
kumkabili (1Samweli 17:37,17:45 – 48). Aliweza
kutotupa ujasiri kwa imani yake katika Bwana.
Mfano wa
Petro Alitupa Ujasiri
Akaanza Kuzama (Mathayo 14:22 – 30)
1.
Alisikia Neno la Yesu “Njoo”
2.
Shetani akanguruma kwa kumwonyesha
upepo
3.
Alipoangalia upepo akatupa
ujasiri, akaanza kuzama
4.
Angeweza kutotupa ujasiri kwa
kuzidi kumtazama Yesu aliyemwita “Njoo”
Wana wa
Israeli Walitupa
ujasiri Hawakuingia Kanani (Hesabu 13:27 – 30,23 – 25)
1.
Waliona majitu
2.
Wakajitazama
wao walivyo, badala ya kumtazama Mungu aliye
pamoja nao.
3.
Walipotazama majitu yalivyo,
Shetani akanguruma wakatupa ujasiri
4.
Wangemtazama Mungu kama Daudi
wasingetupa ujasiri
FAIDA ZA UJASIRI
1.
Kuweza kupokea ahadi kinyume na
mazingira magumu yanayoonekana.
2.
Kuweza kusimama mbele za Shetani
na kumshinda kwa kutumia silaha za kiroho
3.
Kuzalisha matokeo katika mazingira
tatanishi,
Ujasiri
una thawabu, Una matokeo
Usiutupe
BLESSED BE THE NAME OF THE LORD GOD, I REALLY NEEDED THIS LESSON. BLESS YOU PASTOR.
ReplyDeleteAmen. Asante Naomi kwa Kusaidika kwa Ujumbe huu.
ReplyDelete