Thursday, June 26, 2014

Amefanywa Sifuri Usimwogope



Apekduomai

Akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.”
(Wakolosai 2:15)
Neno la Kiyunani kuzivua hapa yaani, “Apekduomai” maana yake ni kuziharibu.  Enzi na mamlaka hizi ni mfumo wote wa mashetani na ngazi zao, kama ilivyoandikwa katika Waefeso 6:12. Hapa imeandikwa kushindana kwetu si juu ya damu na nyama, bali juu ya falme, mamlaka,wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya. Hawa wote wamevuliwa, wameharibiwa.
Mashetani wote wamevuliwa uwezo wa kuhukumu na kuwashika wanadamu kwa kutumia Sheria iliyotutaka tuhukumiwe kwasababu ya dhambi.
Neno linguine linalofanana na hili kwa Kiyunani ni Katageo.

Maana ya neno hili ni: Kufanya sifuri kufanya si kitu, kunyang’anya silaha, kupoozesha.

Wazo Kuu
Kwa njia ya msalaba, mashetani wote walio popote; wamenyang’anywa silaha, wamefanywa sifuri, wamefanywa si kitu, wamepooza!

Tunapotumia Neno la Mungu au jina la Yesu dhidi yao, udhihirisho unatokea wa kuharibiwa kwao. Tayari wameharibiwa, sisi kama waliomwamini Yesu tunadhihirisha kuharibiwa kwao.

SOMA TENA, OMBA  NA KUTAMKA MANENO HAYA KABLA YA KUANZA KAZI ASUBUHI, PIA KABLA YA KULALA TAFAKARI TAMKA NA SHIRIKISHANENI KATIKA KIKUNDI NA IBADA YA NYUMBANI.

1 comment: