Saturday, June 28, 2014

Unaweza Kupokea




Hatua za Kupokea Toka kwa Mungu
Kwa sababu hiyo nawaambia , Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu
(Marko 11:24)
Kupokea katika andiko hili kumegawanyika sehemu mbili:
1. Amini Unapokea
Uombapo saa hiyo hiyo unapokea katika ulimwengu wa roho, ulimwengu war oho hauna muda kila kitu ni sasa  unapokea sasa, ila ulichopokea  hakionekani katika ulimwengu wa mwili, ulimwengu wa mwili una muda.
2. Nayo Yatakuwa Yako
Ulichopokea sasa, hakionekani katika muda huu, lakini kipo ni chako rohoni kwa Neno la Mungu, unacho! Yatakuwa yako maana yake yatadhihirika. Ulichopokea tayari ROHONI kitadhihirika KATIKA MUDA WA MWILINI, ila unacho tayari.
ZIFAHAMU HATUA HIZI
1. Lifahamu Neno Husika:  Neno la Mungu ndilo linatupa mahitaji yetu. Kama ni ugonjwa linauponyaji wetu (1Petro 2:24). Kama ni laana lina Baraka zetu (Wagalatia 3:13). Kama ni kutoweza neno ni kuweza kwetu (Yohana 15:5, Wafilipi 4:13).  Chochote unachohitaji tafuta Neno husika lililonacho hata kama ukioni.  Uwe na “note book” na andika hatua ya kwanza HITAJI NA NENO LAKE.
2.Yashike Yatarajiwayo kwa Hilo: Unachotaka kidhihirike kipokee sasa toka kwenye hilo Neno kwa kukiomba. Sema kwa mfano, “Baba kwa jina la Yesu naomba nitie nguvu nimalize mtihani maana imeandikwa nayaweza yote katika yeye anitiaye nguvu (Wafilipi 4:13). Baba unanitia nguvu kwa Neno hili sasa. Nayo yanakuwa yangu nauona udhihirisho natiwa nguvu”.
3.Usifungwe na Mazingira: Baada ya kuomba hivi unaweza kuona udhaifu ndio unazidi! Usemeshe, mara nyingine uamuru uondoke na kuamuru Neno uliloomba ambalo umesha lipokea litokee kwa jina la Yesu. Kipengele hiki ni cha vita ya imani. Ambayo hupiganwa kinyume na mazingira yanavyoonyesha. Yesu aliongea na upepo, mazingira yakabadilika (Mathayo 8:26).
4.Tenda Jambo: Kuamini maana yake ni kutenda Jambo fulani nje kutokana na jibu ulilokwishapokea kiroho. Kutenda imani ni pamoja na KUSHUKURU ulilopokea moyoni kabla hujaona mwilini katika muda. Kuamini pia ni KUSEMA yasiyooneka, ambayo tayari umeyapokea kana kwamba yameonekana (2Wakorintho 4:13).
5.Ishi kwa Upendo: Imani inazaa matunda na kutenda kazi ndani ya upendo (Wagalatia 5:6).  Imani inaishi kwa upendo. Upendo ni kutenda kama Mungu asemavyo (Yohana 14:21,23).  Upendo ni kumfanyia kitu mtu ambacho ungependa ufanyiwe (Mathayo 7:12). Upendo ni kuongozwa na Roho Mtakatifu kitabia (Wagalatia 5:22). Utendapo tendo la imani, kwa mfano kuomba lazima uwe na upendo yaani kusamehe (Marko 11:25). Kama unatenda tendo la imani la kutoa sadaka lazima liambatae na upendo wa kusamehe ili lizae. Wakati utendapo tendo lolote la imani, lazima mahusiano yako na Mungu na watu yawe ya upendo.
SOMA HATUA HIZI NA KUZIRUDIA, KISHA ZITUMIE KATIKA MAHITAJI YAKO, UTAONA MAJIBU

No comments:

Post a Comment