Katika Waebrania 12:1-2, maandiko yanaonyesha tunazungukwa na wingu la mashahidi wa imani (Waebrania 11).
*Tunazungukwa na mashahidi wanaoshangilia.
*Hawa ni mashahidi wa imani walioshinda kwa imani ambayo na sisi tunayo.
*Bila shaka ni mashahidi wanaoshangilia mbio zetu za imani katika ulimwengu wa roho.
MAMBO YATUPASAYO KATIKA MBIO ZA IMANI
1.Kuweka kando kila mzigo mzito (ogkos), yaani chochote kinachokulemea usiwe na spidi ya mambo ya kiroho. Kama ni magazeti, huzuni nk, weka kando kwa jina la Yesu, uwe mwepesi.
2. Dhambi ituzingayo upesi (hamartia), yaani dhambi rahisi kuifanya. Isemeshe kwa jina la Yesu na kuiweka kando, uwe mwepesi.
3.Tupige mbio kwa saburi (agon), yaani tupigane, tusijirahisishe, tung'ang'anie.
Haya yote tuyafanye katika mashindano yaliyopo mbele yetu. Mashindano ya kusimamia imani zetu hata mwisho.
Nanga yetu inayotufanya tusikose mwelekeo ni KUMTAZAMA YESU, si kitu kingine! Tufanyapo haya imani zetu zitashinda, tutamwona Mungu. Usichoke kukaa katika imani, utauona mwisho mwema, unashangiliwa na waliotangulia!
No comments:
Post a Comment