Kitu Sahihi Moyo Sahihi
Kuhusu mfalme Amazia maandiko yanasema, “Akafanya yaliyo ya adili machoni pa
BWANA lakini si kwa moyo mkamilifu.” (2Nyakati 25:2).
TUNAJUFUNZA MAMBO
YAFUATAYO TOKA ANDIKO HILI
1. Mtu anaweza kufanya kitu kizuri lakini moyo wake ni mbaya
Mfano: Kutoa sadaka au kuomba ili aonekane na watu. Vitu
hivyo ni vizuri ila moyo hauko vizuri.
2. Mtu anaweza kufanya kitu kisicho sawa lakini moyo wake uko
sawa
Mfano: Wakati wa kazi
mtu kuanza kuomba na kusoma Neno.
Kuomba na kusoma neno ni kitu kizuri kutoka moyo mzuri, ila yampasa
amalize kazi kwanza, au aombe taratibu huku akiendelea na kazi na si kuacha
kazi na kuomba . Mtu wa namna hii anatakiwa ashauriwe zaidi ya kulaumiwa tu, ni
mtu mzuri ila anakosea kutumia mambo mazuri aliyonayo.
3.Mtu anaweza kufanya kitu kizuri na moyo wake uko vizuri
Mfano: Mtu anaweza kuomba au kutoa sadaka kwaajili ya
kujulikana na Mungu si wanadamu. Huu ni moyo mzuri unaoambatana na matendo mazuri. Huyu anatakiwa atiwe moyo
aendelee kutenda vema.
4.Mtu anaweza kufanya kitu kibaya na moyo wake uko vibaya
Mfano: Mtu anaweza kumsema mtu vibaya kwasababu anamchukia
moyoni. Huyu anapaswa aonywe kwa kutumia Neno la Mungu liwezalo kubadilisha
moyo.
KITU KIZURI TUFANYACHO
KIAMBATANE NA MOYO MZURI
Usifanye kitu kizuri kwa mtu wakati nia au moyo wako ni
mbaya. Mfano usiende hotelini kumnunulia mtu chakula, wakati moyoni unataka
kuona jinsi anavyokula haraka haraka!
Fanya kitu kizuri kwa moyo mzuri.
Mpeleke kula kwasababu unataka ashibe. Usianze kufanya semina
kwasababu hutaki watu waende semina nyingine inayoanza. Semina unayoanza ni
kitu kizuri ila nia yako au moyo wako haupo vizuri una mashindano. Chochote
tufanyacho kizuri kiambatane na moyo mzuri.
AMAZIA ALIFANYA MAMBO MAZURI.
INAWEZEKANA ALIMWABUDU MUNGU, ALIOMBA, ALIWAPA MASKINI SADAKA. PAMOJA NA HAYA YOTE YALIYO MEMA HAKUFANYA KWA
MOYO MKAMILIFU. KABLA HATUJAFANYA JAMBO, TUJIULIZE KWA NINI TUNAFANYA? Ni
kwaajili ya upendo kwa watu na Mungu. Ni
kwaajili ya kumtii Mungu au kupendeza watu? Tuipime mioyo kabla ya matendo. Kwa
kufanya hivi tuyatendayo yatapata kibali kwa Mungu. Mungu anataka tuyafanyayo nje
yawe sawa ndani ya mioyo yetu.
No comments:
Post a Comment