Friday, November 4, 2016

KUSUDI LETU-WordDrillers

Leo tena kusudi la "WordDrillers" limehuishwa ndani yangu.


I. KUKAA KATIKA NENO (Yohana 5:24, 8:51-52)
Tunakaa katika Neno na kumjua Mungu yukoje
Tunabadilika siku kwa siku, toka utukufu hata utukufu, sawasawa na Neno lake.

II. KUMWABUDU MUNGU (Yohana 4:23, 1Wakorintho 6:19-20)
Tunamwabudu tunayemjua kwa Neno lake.
Mwenendo wetu unaendana na kweli yake tunayoijua. Hivyo tunakuwa waabudu wa kweli.
Neno linatutenga katika Roho Mtakatifu kwaajili ya Mungu tu, hii ni ibada.

Mioyo yetu imeshikwa na ufahamu wa Mungu kwa Roho katika Neno, sadaka za kuimba, mali, muda na fedha tunazitoa kwa tunayemwabudu toka mioyoni mwetu, kwa ufunuo wa neno lake yukoje katika maisha yetu. Hii ni ibada.

Tunailinda miili yetu kwa Neno lake,  isitumiwe kutenda dhambi, bali itumiwe kutenda neno ili kutakaswa. Hii ni Ibada.

Tunaishi na ndugu zetu katika Bwana kama tunavyoishi na Mungu kwa kuwa wameumbwa kwa mfano wake. Hii ni ibada.

Tunawekwa huru na kila adui ili tumwabudu Mungu pasipo hofu (Luka 1:74).

III.KUUFIKIA ULIMWENGU (Marko 16:15-20)
Mungu tunayemjua kwa Neno lake.
Mungu tunayemwabudu kwa Neno lake.
Mungu tunayeishi naye kwa Neno lake.
Mungu anayetutenga na kutubadilisha kwa Neno lake.

Tunampeleka duniani kwa Neno lake.

No comments:

Post a Comment