HUDUMA YA YESU
SASA
Msalaba ulifungua mlango wa Yesu kuingia mbinguni kufanya
huduma ya Kikuhani. Msalabani Yesu alijitoa sadaka, mbinguni Yesu anatuhudumia
kwa sadaka aliyoitoa msalabani.
I. HUDUMA YA KIKUHANI
NI NINI?
Hii ni huduma inayohusisha mambo yafuatayo:
1. Uwakilishi kwa Damu yake2.Uunganishi
kwa damu yake 3. Kumkaribia Mungu kwa damu yake 4. Kuwashika watu na Mungu na
kuwaweka pamoja kwa njia ya sadaka yeke mwenyewe.
II. AINA ZA UKUHANI
1. Ukuhani wa Haruni
Huu ulikuwa ni ukuhani wa mfano wa
ukuhani wa kweli wa milele mbinguni. Ulitumia sadaka za wanyama. Patakatifu pa
duniani, na mambo mengine ya kibinadamu.
2. Ukuhani wa Melikizedeki
Huu ni ukuhani halisi wa milele wa
Yesu. Unatumia sadaka ya Yesu mwenyewe, patakatifu ni pa mbinguni, damu ya
Mungu,huu ndio ukuhani halisi uliokamilika.
III. HUDUMA YA YESU WAKATI HUU
Huduma ya uwakilishi au uunganishi ya
Yesu Kristo wakati wa sasa inaonekana kwa Yesu kuwa kama ifuatavyo:
MJUMBE (Mediator)
Yesu ni daraja la watu wote kumfikia
Mungu. Binadamu wote hupitia kwake ili wakutane na Mungu (Yohana 14:6). Mtu
anapotubu dhambi anatubu kupitia Yesu Kristo nasadaka yake aliyoitoa msalabani.
Ni kama vile Yesu anamshika mtu huyo na kumuunganisha na Mungu, Yeye Yesu akiwa
katikati (Ayubu 9:33, 1Timoteo 2:5, Waebrania 8:6).
MDHAMINI (Surety)
Yesu ni mdhamini wa agano jipya. Ni uhakika
wa kutimia kwa agano jipya. Ahadi zote za Mungu katika agano jipya
zimedhaminiwa na Yesu ili zitimie, dhamana yake ni Yesu na damu yake. Kama vile mtu asipolipa pesa dhamana yake
hukamatwa, agano limeshikwa kwa mdamini Yesu (Waebrania 7:22). Lisipotimia ‘Yesu
atakamatwa’.
WAKILI (Advocate)
Yesu mbele za Mungu ni mtetezi wetu
(1Yohana 2:1-3). Neno Mwombezi kwa Baba katika maandiko haya tafsiri yake ni wakili. Wewe kama mwamini ukikosea na
kutubu dhambi, Yesu anasimama kama shahidi wa kusamehewa dhambi zako, maana
alimwaga damu yake uokolewe.
MWOMBEZI (Intercessor)
Waebrania 7:25, inaonyesha Yesu ni
mwombezi, Tafsiri rahisi ni anayekumbusha.
Yesu anaweza kutuokoa kabisa, andiko hili ndivyo linavyosema. Tumeokolewa roho,
tunafanywa upya nafsi, na siku moja miili yetu itabadilika. Yesu ndiye
anayesimama mbele za Mungu kuhakikisha ukamilifu wetu umetimia, tunafanana naye
kitabia, hata tutakapoingia mbinguni. Yeye anayatumia maneno yetu, ibada zetu,
sifa, shukrani mbele za Mungu, UKIRI WA IMANI, hata udhihirisho utakapotokea
duniani kwa neema.
(Waebrania 4:14-16)
WAKATI MWINGINE TUTAENDELEA KUMTAZAMA
YESU KAMA KUHANI MKUU NA KUHANI WA ZAMU.
No comments:
Post a Comment