Friday, November 21, 2014

Huduma ya Mwinjilisti



                                  Wainjilisti (Euaggelistes)
(a)  Mwinjilisti ni huduma ya muhimu sana katika Agano Jipya. Agano Jipya ni Agano la habari njema za kuja, kuishi, kufa, kufufuka, kupaa, kuketi na kurudi kwa Yesu. Ofisi ya mwinjilisti imeshika kazi hii yote.
(b)  Mwinjilisti ni mjumbe wa habari njema kama vile malaika (Luka 2:10).
(c)  Mwinjilisti huenda sehemu moja na nyingine kutangaza habari za Yesu kutoka kanisani, Hupelekwa na kanisa.
(d)  Hitaji kubwa la mwinjilisti ni watu kutubu na kuokolewa, pia kutoka katika nguvu za giza.
(e)  Huduma hii inahitaji huduma za masaidiano; huduma ya maombezi, usimamizi, kukirimu, maongozi; Pia huduma za uongozi kama uchungaji pamoja na ualimu.
(f)   Mwinjilisti wa mfano katika Biblia ni Filipo (Matendo 8)
(g)  Mshirika yeyote anaweza kufanya kazi ya mwinjilisti hata kama yeye siyo ofisi yake. Paulo alimwambia Timoteo afanye kazi ya Mwinjilisti (2 Timoteo 4:5).
(h) Karama kuu katika huduma hii ni karama za nguvu (karama ya Imani, uponyaji, miujiza, pia karama ya unabii kama apendavyo Roho)
(i)   Mwinjisti hutangaza habari za Yesu, tofauti na mwalimu huelezea au hufafanua neno.  

Huduma hii ni ya muhimu kama huduma nyingine zote, ingawa kidini inaonekana ni ndogo, lakini katika Kristo ni ya muhimu, maana kazi ya msalaba inaonekana maana yake katika uinjilisti: Kusamehewa, Kuhesabiwa haki, Kufunguliwa toka pepo wabaya, nk.

No comments:

Post a Comment