Sunday, November 23, 2014

Huduma ya Mchungaji



                                                                                               Mchungaji  (Poimen)
(a)  Mchungaji ni msaidizi wa kondoo, huduma hii ni yakusaidia kondoo (Poimen). 

(b)  Mchungaji ni mzee (Presbuteros). Nyakati za Biblia mzee alikuwa ni mtu yeyote katika kanisa mwenye sifa za uongozi wa huduma tano(mtume, nabii, mwinjilisti na mwalimu). Mzee pia aliweza kuwa katika huduma mojawapo ya masaidiano. Kwa upande mwingine alikuwa ni mtu mzima kiumri aliyekuwa kiroho na kimaadili. Mchungaji naye ni mzee(presbuteros) kihuduma alikuwa juu ya wengine wote wenye sifa hizi katika kundi. 

   Ingawa mtume alipokuwepo katika kundi alikuwa ni mzee mwenye sifa na, hata hivyo kwasababu ya utaratibu ilipaswa ajitiishe kwa mchungaji katika kuongoza kundi. Mitume walioonekana wazee katika maandiko ni Yohana (2Yohana 1) na  Petro (1Petro 1:1), Petro alijiita mzee (1Petro 5:1), wote hawa walikuwa ni mitume na wachungaji.

(c)  Mchungaji ni mwangalizi wa roho au askofu (Episcopos). Askofu kwa msingi lilikuwa ni neno lenye maana ya mwangalizi wa roho. Baadaye lilitumika kwa mzee mmoja aliyekuwa na mamlaka juu ya wazee wengine walioisimamia kanisa la mahali. 

(d)  Mchungaji ni mlezi, hufanya ulezi kwa:
1.   Kusimamia kundi (kutawala), (1Wakorintho 12:28)
                             -  Ana huduma ya masaidiano ya kusimamia.
2.   Kulisha kundi au kondoo, kwa neno la wakati (revelation) (Zaburi 23)
3.   Kuelekeza kundi au kondoo (Zaburi 23-Fimbo)
4.   Kujali kondoo, kuguswa na hisia zao na kuwa nao (Mathayo 18:12)
5.   Kuponya kondoo
                           -Ana huduma ya masaidiano ya rehema kama Msamaria(Luka 10:37)
6.   Kulinda kundi (Zaburi 23- Gongo) hulinda kwa :
-      Mafundisho ya  msingi (doctrine) na mafunzo(training).
-      Maombezi; ya kuhifadhi, ya kukuuza, ya kutegemeza, ya kupigania kondoo.
-      Upako wa ulinzi katika ofisi yake. Mchungaji ana macho au roho ya ufahamu inayojua kiwango cha kiroho cha kondoo, inayoona au kuhisi hatari kwa kundi nk
-      Maonyo; mchungaji huonya kondoo na kuwa
-      Nidhamu ya kanisa:mchungaji husimamia nidhamu ya kanisa:
·     Kidole kikivimba hutibiwa kipone, ila kikioza hukatwa mwili mzima usioze.
·       Katika kanisa kuna watu wa kutibiwa, wengine wakukatwa ili mwili au kanisa lisiharibike. Hii ni nidhamu ya kanisa.
7.   Yapasa aheshimiwe na kundi (1Timoteo 5:17).

1 comment: