Aina za Huduma
Kwaajili ya kuelewa
vizuri tutaangalia huduma katika makundi matatu
1. Huduma za viongozi (karama za Yesu)
2. Huduma za masaidiano
3. Huduma za kanisa
Huduma
za Uongozi
Huduma hizi zipo tano ni Yesu mwenyewe huzitoa,
ni karama za Yesu. Karama za Roho hazipo wakati wote huja kwa uhitaji maalumu,
lakini hizi ni ofisi za wakati wote.
1.
Mitume (Apostolos)
(a) Aliyetumwa kuwakilisha ufalme kama balozi
(b) Ni mwanzilishi na mweka msingi wa kanisa jipya au
makanisa mapya, huweka msingi kwa kufanya yafuatayo:
(1) Huhubiri
(2) Hufundisha (3) Hufunza viongozi wapya (4) husimamia mafundisho
sahihi ya Imani.
(c) Mara nyingi huanza kwa kupitia huduma nyingine na
yenyewe ya kitume kuonekana baadaye (Matendo 13:1-3). Mtume lazima awe amekuwa
kiroho na kihuduma, kabla ya kuanza utume. Mfano TL Osborn alikuwa mchungaji
kabla ya utume. Reinherd Bonnke alikwa Mchungaji kabla ya uinjilisti wa
kimishionari. Paulo alikuwa mwinjilisti na mwalimu kabla ya kuanza utume
(Matendo 13).
(d) Mitume huitwa na Yesu na kupelekwa na kanisa.
Aina za Mitume
(1) Mitume 12 (mitume wa mwanakondoo)
(2) Mitume wa kupaa (Walioitwa baada ya Yesu kupaa,Waefeso
4:10-13). Hoja kwamba leo hakuna mitume ni uongo, maana uhitaji wa injili
kufika maeneo yasiyofikiwa ni mkubwa kuliko wakati wowote.
(3) Mitume wa uongo
(e) Mitume hufanya kazi ya kimishionari, huvuka mipaka
ya kitamaduni na kuhubiri injili, huanzisha makanisa, kuandaa na kuweka viongozi
maeneo tofauti na utamaduni wao, kama vile lugha nk.
(f) Karama kuu zifanyazo kazi pamoja na huduma katika
huduma hii ni ualimu, uinjilisti, miuijiza, usimamizi (maongozi) na hufanya
kazi karibu na manabiii au wao wenyewe mitume huwa manabii.
(g) Mtume lazima awe mwinjilisti, huduma ya mwinjilisti hufanya kazi karibu na mtume. Naweza kusema hakuna mtume asiye mwinjilisti. Katika hali ya kidini huduma ya mwinjilisti imedharauliwa, lakini ni huduma muhimu sana agano jipya, maana ni agano la injili ya Yesu Kristo.
(h) Huduma hii haipo kwa wanaume tu, ni kweli mitume wa mwanakondoo, wale 12 walikuwa wanaume tu. Baada ya Yesu kupaa alitoa mitume wengine wanaume kwa wanawake; mfano Warumi 16:7, inaonyesha mtume mwanamke aliyeitwa Yunia.
(i) Dalili nyingine ya huduma hii, mitume huwa mababa wa viongozi wengi wa kiroho, kwa mfano Paulo alikuwa baba wa viongozi wengi wa kiroho, kwa mfano wa Mozes Kulola.
No comments:
Post a Comment