Friday, October 3, 2014

Utauwa na Kuridhika

DAWA YA KUPENDA PESA
Kuridhika ni kufurahia mahali ulipo kwasababu ya Yesu, hata kama unahitaji vingine, furahia ulivyonavyo. Shukuru kwa ulichonacho kabla ya kupata ambacho huna. Hii itakujengea moyo wa kuridhika.

Utauwa ni uungu, tunahitaji utauwa na kuridhika, hii ni faida kubwa. Maandiko yanasema, "Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa, kwa kuwa hatukuja na kitu duniani, Tena hatuwezi kuondoka na kitu, Ila tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo. " (1Timoteo 6:6-8).

Ili mali iwe na faida kwetu tunahitaji uungu, yaani utauwa pamoja na kuridhika. Bila utauwa na kuridhika ni hasara hata kama tuna mali. Utauwa unampa Mungu nafasi ya kwanza, kuridhika kunatufanya tuwe na amani na kile tulichonacho. Hali hizi mbili hufanya kile tulichonacho tukifurahie, kiwe na faida.
Msitari wa kumi unasema, "Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi" (1 Timoteo 6:10).

Ukisoma msitari wa sita, Saba, nane na Kumi utagundua mlango wa kupenda pesa ni kukosa utauwa na kuridhika. Pesa siyo mbaya, Ila kupenda pesa ndio kitu kibaya. Kupenda pesa kumeshikwa na kukosa utauwa na kutoridhika. Huwezi kuwa na vitu vyote wakati wote, furahia ulipo na ulichonacho, huku ukiishi kiungu, Milango itafunguka kukuongeza.

SIKU MOJA USHUHUDA ULISEMA NA MIMI NDANI YANGU MANENO HAYA, NAAMINI ALIKUWA NI ROHO MTAKATIFU, ULISEMA, "MWANADAMU, ULICHONACHO NI UZIMA WAKO MBELE ZA MUNGU" NILIGUNDUA KUWA PAMOJA NA PESA AU MALI NILIZONAZO NA NITAKAZOKUWA NAZO, MALI YANGU YA KWELI NI UZIMA ALIONIPA YESU; UWEZO WA KUISHI NA MUNGU MILELE! VINGINE NI VYA MUHIMU ILA VINAPITA

No comments:

Post a Comment